Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanawake wa Mikese na Mkambarani mkoani Morogoro, wameiomba
Serikali kuwatatulia kero sugu ya maji iliyodumu kwa muda mrefu kiasi
cha kusababisha ndoa zao kuingia kwenye migogoro kutokana na kutumia
muda mwingi kutafuta na kuziacha familia bila kuwa uangalizi wa kutosha.
Wakizungumza na gazeti hili katika Kijiji cha
Fulwe Kata ya Mikese, mkoani Morogoro, Anna Massawe na Justina Eliasi
walisema kero ya maji imekuwa kubwa na wanalazimika kutembea umbali wa
kilometa 15 kila siku kusaka maji.
“Kweli ndoa zetu zipo hatarini kwa kuwa muda
mwingi tunashinda kutafuta maji. Familia inakosa malezi ya karibu ya
mama. Waume nao wanakuwa mbali nasi kwa muda mwingi,” alisema Anna
massawe.
“Kila wakati wa uchaguzi unapofika, ahadi za
viongozi ni kutatua kero ya kukosa maji, wakishaingia madarakani hakuna
anayekumbuka. Maisha haya mpaka lini?” alihoji.
Akizungumzia hali hiyo, Diwani wa Kata ya Mwega,
Jafari alisema Serikali imesikia kilio cha wakazi wa eneo hilo na kwamba
iko kwenye mkakati wa kumaliza kero hiyo.
“Serikali inatambua adha na kero ya ukosefu wa
maji kwenye kata hii, tayari tumeshaunda kamati maalumu ya kufuatilia
tatizo hili. Nadhani muda siyo mrefu tutapata majibu,” alisema Jaffari. Wanawake wa Mikese na Mkambarani mkoani Morogoro, wameiomba
Serikali kuwatatulia kero sugu ya maji iliyodumu kwa muda mrefu kiasi
cha kusababisha ndoa zao kuingia kwenye migogoro kutokana na kutumia
muda mwingi kutafuta na kuziacha familia bila kuwa uangalizi wa kutosha.
Wakizungumza na gazeti hili katika Kijiji cha
Fulwe Kata ya Mikese, mkoani Morogoro, Anna Massawe na Justina Eliasi
walisema kero ya maji imekuwa kubwa na wanalazimika kutembea umbali wa
kilometa 15 kila siku kusaka maji.
“Kweli ndoa zetu zipo hatarini kwa kuwa muda
mwingi tunashinda kutafuta maji. Familia inakosa malezi ya karibu ya
mama. Waume nao wanakuwa mbali nasi kwa muda mwingi,” alisema Anna
massawe.
“Kila wakati wa uchaguzi unapofika, ahadi za
viongozi ni kutatua kero ya kukosa maji, wakishaingia madarakani hakuna
anayekumbuka. Maisha haya mpaka lini?” alihoji.
Akizungumzia hali hiyo, Diwani wa Kata ya Mwega,
Jafari alisema Serikali imesikia kilio cha wakazi wa eneo hilo na kwamba
iko kwenye mkakati wa kumaliza kero hiyo.
“Serikali inatambua adha na kero ya ukosefu wa
maji kwenye kata hii, tayari tumeshaunda kamati maalumu ya kufuatilia
tatizo hili. Nadhani muda siyo mrefu tutapata majibu,” alisema Jaffari.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment