MANISPAA ya Morogoro imeanza zoezi la kuvunja na kuondoa mabango
ya biashara ambayo hayalipi kodi kwa manispaa hiyo, ambapo zaidi ya sh
milioni 370 zinadaiwa kutoka kwa wamiliki wa mabango hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Ofisa Uhusiano wa
manispaa hiyo, Lilian Henerico, alisema manispaa imeamua kuondoa
mabango hayo ili wahusika wanaodaiwa kulipa, ikiwa ni pamoja na kulipa
faini kutokana na kuchelewa kulipa.
Alisema zoezi hilo ni la siku 14 na wameanza na mabango ya makampuni
makubwa na baadaye kuondoa mabango madogo na kwamba hatua zaidi za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao pamoja na kupelekwa mahakamani.
“Mabango tunayovunja na kuyaondoa ni yale yanayodaiwa kodi kwa muda
mrefu na manispaa, zoezi hili ni la siku 14 na tutawapeleka mahakamani
kwa wale ambao pamoja na hili zoezi hawatalipa,” alisema Henerico.
Alisema mabango hayo ni yale ya makampuni makubwa, watu binafsi na
mashirika, ambapo alisema baadhi ya watu binafsi wakati wa zoezi hilo
walianza kulipa huku wakikubali kulipa na faini zao kwa wakati huohuo
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment