CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeitaka serikali
kumnyang’anya mwekezaji wa kiwanda cha sukari Mtibwa rasilimali hiyo
kutokana na kushindwa kuwalipa wakulima na wafanyakazi madai yao.
Diwani wa Mtibwa, Luka Mwakambaya (CHADEMA), alitoa kauli hiyo ikiwa
ni siku chache baada ya Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Antony Mtaka,
kusimamisha uzalishaji wa kiwanda hicho hadi wakulima na wafanyakazi
hao watakapolipwa malipo yao sh bilioni 1.9.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwakambaya ameijia juu Serikali
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na watendaji wake, kwamba hawana uchungu
na maisha ya wananchi wanaonyanyasika ndani ya nchi yao, kutokana na
kushindwa kumuadabisha mwekezaji huyo.
“Wananchi wanashindwa kulipa matibabu ya ndugu zao hospitali ya
Bwagala, wanafunzi wameshindwa kupelekwa shule, wanashindwa kuvaa na
kujikimu wenyewe kwa mahitaji, kutokana na mwekezaji kuhodhi malipo ya
wakulima wadogo wa miwa na mishahara ya wafanyakazi.
“Ninafanya upembuzi yakinifu wa majina ya wastaafu zaidi ya 110
waliokufa bila kupata mafao na haki zao stahili, huku wengine wakiwa
wamelipwa kati ya shilingi 5oo,ooo au milioni moja ijapokuwa wamefanya
kazi zaidi ya miaka 32 na wengine kufukuzwa bila sababu,” alisema
Mwakambaya.
Alisema katika ahadi aliyoitoa Meneja wa kiwanda, Hamad Yahaya, siku
ya mkutano wa hadhara baina ya Mkuu wa Wilaya, Mtaka na wakulima na
wafanyakazi, aliahidi kuingiza fedha hizo, lakini fedha iliyoingizwa
kwenye chama kimoja cha wakulima ni sh milioni 70.
Alisema hali hiyo ni dharau na matusi kwa wakulima na wafanyakazi
wanaoteseka na familia zao nchini kwao, kana kwamba wako Somalia, hivyo
akadai anasikilizia kikao cha kesho na Mtaka kitakuwaje, vinginevyo
wataiomba polisi iwalinde mlangoni kwa mwekezaji watakakoweka mikeka
Chanazo;tanzniaDAIMA
0 comments:
Post a Comment