Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
JUMUIYA ya Serikali za Mitaa (ALAT) Taifa, imeitaka serikali kuu
kutangaza kuzivunja serikali za mitaa iwapo wanaona hazihitajiki
kutokana na kushindwa kuzitambua katika rasimu ya katiba mpya.
Kwamba rasimu hiyo isijadiliwe na irudishwe upya kujadiliwa kwanza na
Watanganyika, ambao hawakupata fursa ya kuijadili kama ilivyofanyika
kwa Watanzania na Wazanzibari.
Mwenyekiti wa ALAT taifa, ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar
es Salaam, Didas Masaburi, alisema hayo alipozungumza na waandishi wa
habari mjini Morogoro.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment