Mratibu wa matembezi ya Dar mpka Moro Bw, Matukio Chumaa akiwa kwenye muonekano wa picha.
.NCHI YANGU; WAJIBU WANGU 11.01.2014 (takribani 200km)Dar es Salaam mpaka Morogoro.
Ndugu
zangu Watanzania, naomba kuwasalimu, katika jina la Mlima mrefu ukaitwa
Kilimanjaro, visiwa vya marashi ya karafuu Zanzibar, Serengeti,
Ngorongoro, mapango ya Amboni, pwani zilizojaa kubwa shani na ardhi
yenye wingi wake gesi na madini, kwa hakika umaskini/ufukara wetu upo
katika fikra zetu.
Kuanzia
tarehe 11.01.2014 Matembezi ya hiyari kwa miguu kutoka Dar es Salaam
mpaka Morogoro yataanza rasmi yakikadiriwa kuchukua siku zisizozidi
kumi, lengo kuu likiwa ni kuhamasisha, kukumbushana na kuenzi Umoja,
Amani na Utulivu kama Taifa moja likaitwa Tanzania ilhali juhudi
yakinifu kuanzia ngazi ya mwananchi mmoja mmoja, familia, kaya, wilaya
mpaka Taifa kujivika jukumu la kufahamu, kupambanua, kudadavua na mwisho
wa siku kushirikiana kupitia njia za makusudi kuhakikisha maliasili na
utajiri wa Taifa hili jadidu unamnufaisha kila Mtanzania, huku masuala
ya Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii, Ujasiriamali na Taaluma yakitiliwa
mkazo pasi kuachwa kando.
Matembezi
haya yanatarajiwa kuwa na vituo kadhaa vikiwemo ; Kibaha, Mlandizi,
Vigwaza, Chalinze, Mikese na kumalizia Morogoro, tunatarajia ndugu zetu
Watanzania tujikimu kwa mahitaji kadha wa kadha tuwapo safarini, Nchi
ikiwa Yetu, Wajibu ukiwa Wetu na UTAIFA tukiuweka na kuutanguliza mbele.
Mpaka
sasa matembezi haya ya hiyari yenye kauli mbiu Nchi Yangu, Wajibu Wangu
: UTAIFA KWANZAhayajapata mdhamini yeyote na maandalizi yote mpaka sasa
ni kufikia lengo la matembezi kama Tanzania iliyo moja bila kujali
itikadi, imani, dini, asili ama hata tofauti za kiuchumi miongoni mwetu
na kuangaza katika Tanzania yenye kutoa nafasi kwa kila Mtanzania.
Kwa
hakika maandalizi ya msingi yamekamilika na tarehe 11.01.2014 ndoto
yetu ya kufanya matembezi ya hiyari yatafikisha ujumbe ulio wa Amani na
Ustawi wa Taifa letu itachukua nafasi na kuwa halisia.
Nchi Yangu, Wajibu Wangu : UTAIFA KWANZA
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma
+255-772-54-55-62/784-311056,
Barua Pepe: kwetutanzania@yahoo.com, Ukurasa: www.facebook.com/kwetutanzania
0 comments:
Post a Comment