Home » » Serikali yawanyang`anya mashamba wawekezaji

Serikali yawanyang`anya mashamba wawekezaji

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera
 
Serikali ya Wilaya ya Mvomero mkoani hapa imenyang'anya ekari 500 za mashamba na kurejesha kwa wananchi baada ya kubaini kuwa uwekezaji wake ulikuwa wa udanganyifu.
Mkuu wake, Anthony Mtaka alisema wameamua kunyang'anya mashamba hayo yaliyopo kwenye msitu wa Kata ya Kibaoni Tarafa ya Mlali kutokana na kukumbwa na migogoro ya ardhi na kusababisha madhara, wananchi kukosa maeneo ya kuendeshea shughuli za kijamii na maendeleo kwa wananchi.

Akitoa maelezo ya dhamira ya serikali kufanya hivyo,  Mtaka,  alisema wawekezaji wengi wanakimbilia Mvomero kwa lengo la kujinufaisha badala ya maendeleo kwa wananchi na kuwa  kichocheo kikubwa cha migogoro ya ardhi.

“ Sheria zimewekwa ili zifuatwe na kuheshimika hivyo sitosita kuwafutia hati miliki zao wawekezaji wote waliojipatia maeneo kiholela  na kuacha wananchi wanakosa maeneo ya kilimo,”alisisitiza.

Alisema haiwezekani wawekezaji wafike kwenye mashamba na kujimilikisha kiholela huku wananchi wakikosa   maeneo ya kulima.

Alisema hakuna sheria ya ardhi inayosema pori la kijiji ni mali ya mwekezaji anayetaka kumiliki kwa maslahi yake binafsi badala yake wananchi wakubaliane na kumpatia kwa maendeleo na si  vinginevyo.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa