Miss
Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika
kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa
Maria, Sista Flora Chuma.
Miss
Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Jana amejumuika na watoto
yatima wa kituo cha Mgolole kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa
Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss
Kanda ya Mashariki, Missa Clara Pamoja Sabra Islam Miss Morogoro 2013 .
Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa. Aliongozana na Wazazi wake
pamoja na ndugu jamaa na marafiki zake.

Watoto
wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria
cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja jana
walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss Tanzania, Happiness Watimanywa
aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss Tanzania pamoja na wazazi wake
ndugu na jamaa wake wa Karibu.
Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundega Akiwa na Katibu wa Miss
Tanzania, Bosco Majaliwa jana walipoongozana na Miss Tanzania 2013
Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha
Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria Cha Mkoani
Morogoro
Ndugu
na marafiki wa Miss Tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa
alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro..
Miss Tanzania 2013, Hapiness Watimanywa Kulia akiwa na mama yake mzazi
Wazazi
wa Miss Tanzania Bwana na Bibi Watimanywa katika picha pamoja na mtoto
yatima wa Kituo cha Mgolele walipomsindikiza mtoto wao ambaye ni miss
Tanzania 2013 Hapiness Watimanywa alipoenda kusherekea Sikukuu ya
Chrismass pamoja na watoto hao jana ambapo amepata mapokezi mazuri
kutoka kwa uongozi wa kituo hicho.
Miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa akiwa pamoja na wadogo zake wakiwa wamewabeba watoto katika yatima wa kituo hicho
CHANZO : MATUKIO BLOG
0 comments:
Post a Comment