Mvomero.Mkuu wa Operesheni wa Polisi, Paul
Chagonja amewasili eneo la mapigano kati ya wakulima na wafugaji vijiji
vya Hembeti na Kambara, Wilaya ya Mvomero, yaliyosababisha mauaji ya
watu sita.
Hata hivyo, Chagonja baada ya kuwasili aliwataka
wananchi kumaliza migogoro kwa amani na utulivu, huku akiwasisitiza
kutumia njia ya mazungumzo badala ya kujichukulia sheria mkononi.
Chagonja aliyeongozana na maofisa wengine kutoka
Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, alisema kutokana na vurugu hizo
watu sita wamefariki dunia na kujeruhi 30.
Alisema polisi wameimarisha ulinzi na kwamba, hali
kwa sasa ni tulivu hivyo wananchi waendelee kuimarisha umani kufuata
sheria kupata haki zao.
Aliongeza kuwa licha ya kusababisha vifo na majeruhi, vurugu hizo zimeathiri shughuli za uchumi na huduma za jamii kusimama.
kama shule hasa ukizingatia kwa sasa wanafunzi wa
kidato cha nne wanafanya mitihani na kwamba katika vijiji hivyo wapo
wanafunzi wa kidato cha nne ambao naweza kushindwa kwenda kufanya
mitihani yao wakihofia vurugu zinazoweza kujitokeza wakiwa shuleni ama
wakati wa kwenda shule.
Awali akizungumzia vurugu hizo, Kamanda wa Polisi
mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilitokea
Novemva 4 mwaka huu saa 10:00jioni baada ya ng’ombe 300 wa Semwako
Mtunda ambaye ni mfugaji wa jamii ya kimasai kutoka kitongoji cha Mpapa
Hembeti kuingiza ng’ombe katika mashamba ya wakulima wanne na kuharibu
mazao mbalimbali.
Alisema ng’ombe hao walichukuliwa na kikundi cha
ulinzi wa jadi cha Mwano na kupelekwa kwenye kijiji cha Hembeti ,wakiwa
katika ofisi ya kijiji wakiendelea na majadiliano kwa pande zote mbili
kikundi cha ulinzi wa jadi cha Mwano kugoma na kudai kupewa kiasi cha
sh.3 milioni na mmiliki wa ng’ombe hao alikubali kulipa lakini walinzi
kugomea kiasi hicho cha fedha.
Alisema wakati wakiendelea na madailiajo hayo
ndipo walipotokea wafugaji wa jamii ya kifugaji wakiwa na silaha za moto
kwa ajili ya kutaka kuchukua mifugo na katika harakati hizo za mapigano
kulipelekea majeruhi tisa na kupelekea mtu mmoja Yusuf Mbutu mkulima wa
kijiji cha Mkindo kufariki dunia majira ya jioni
Ilielezwa kuwa Novemba 6 mwaka huu, saa 4:00
asubuhi kulitokea mapigano mengine katika eneo la kijiji cha
Mpapa-Kigulukilo kati ya kikundi cha Ulinzi wa jadi cha Mwano na
wafugaji wa kimasai hali iliyopelekea kifo cha watu watano na majeruhi
28 kati yao wawili wafugaji na watatu kutoka kikundi cha ulinzi wa jadi
cha Mwano.
Chanzo;Mwananhi
Chanzo;Mwananhi
0 comments:
Post a Comment