Home »
» Bodaboda za kilimo zaja
Bodaboda za kilimo zaja
|
|
KAMPUNI ya General Business (GB) ya mjini hapa, imeingiza aina
mpya ya pikipiki kutoka nchini China ambazo zitatumika kwa ajili ya
wakulima kuongeza uzalishaji wa zao la mpunga na mahindi.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi
Mtendaji wa GB Morogoro, Peter Mpembwa, alisema kampuni hiyo imeamua
kuingiza pikipiki hizo ili kumpunguzia gharama za uzalishaji na
kumwezesha mkulima kuzalisha kwa tija.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, pikipiki hizo ikiwemo aina ya GN,
Escort na Elegant, ambazo tayari zipo mjini hapa, zimeundwa katika
muundo wenye uwezo wa kukabiliana na mazingira ya vijijini kwa ajili
ya kilimo.
‘‘Baada ya kuona serikali imekuja na sera ya 'Kilimo kwanza' yenye
dhamira ya kuinua kilimo nchini, GB ilifanya mazungumzo na kampuni za
nje ikiwemo Kampuni ya China ya GS-Group ili tupate nyenzo rahisi
katika kumpunguzia gharama mkulima...wakaja na aina hii ya pikipiki,”
alisema Mpembwa.
Kuhusu mpango mkakati wa kampuni hiyo, Mpembwa alisema zaidi ya
ekari 500 zinatarajiwa kuanza kutumika kuzalisha zaidi ya tani 300 za
mpunga ili kuuwezesha mkoa kuzalisha mpunga utakaotosheleza mahitaji ya
ya chakula nchini.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
0 comments:
Post a Comment