MWENYEKITI wa Chama cha Wakulima (TASO) Kanda ya Mashariki, Mohamed
Mzee amesema wizara tatu zinazodaiwa zaidi ya Sh milioni 56 ikiwamo
Wizara ya Chakula, Kilimo na Ushirika zimechangia chama hicho kutofikia
malengo katika kufanikisha maonyesho ya mwaka huu.
Alizitaja wizara nyingine kuwa ni Viwanda na Biashara na Wizara ya Mifugo.
Mzee alisema madeni hayo yamechangia chama hicho kushindwa kufikia malengo hasa katika kipindi hiki cha maonyesho ya wakulima ya Nanenane ambayo yalianza jana mkoani hapa.
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Manispaa ya Morogoro jana.
Madeni hayo yamechangia kukwamisha baadhi ya malengo ya TASO ikiwamo kuweka lami kwenye barabara ndani ya uwanja huo ili kupunguza vumbi, alisema.
Aliyataja malengo mengine kuwa ni kuongeza mabomba ya maji, taakatika barabara mbalimbali na kumalizia ujenzi wa ukuta katikasehemu ambayo haina ukuta.
Mwenyekiti huyo alisema TASO pia inadai Sh milioni 250 kutoka bodi mbalimbali na halmashauri.
Alizitaka kuhakikisha zinalipa madeni hayo haraka kusaidiamaonyesho hayo.
Maonyesho hayo ya kanda ya mashariki yanashirikisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro ambako kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Kilimo kwanza, kuzalisha mazao ya kilimo na mifugo kwa kulenga soko’.
GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment