Home » » MAHAFALI YA TANO YA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO

MAHAFALI YA TANO YA CHUO KIKUU CHA KIISLAMU CHA MOROGORO


Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro,Hajjat Mwatumu Malale (katikati) akiwa ameketi jukwaani na viongozi wengine wa Chuo Kikuu hicho,wakati wa sherehe ya mahafali ya tano ya Chuo hicho yaliyofanyika siku ya Novemba 17, mwaka huu.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro ( MUM) Hajjat Mwatumu Malale ( kushoto ) akimkabidhi mmoja wa mwanafunzi bora kimasomo wa Chuo hicho ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja wakati wa sherehe ya mahafali ya tano yaliyofanyika siku ya Novemba 17, mwaka huu kwenye viwanja vya Chuo Kikuu hicho.
Mwandishi wa Habari wa kituo cha Televisheni na Redio Abood, Abeid Dogoli ( wa kwanza kushoto) na wezake Mohamed Mohamed ,ambaye ni mfanyakazi wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) na Redio Zanzibar ,sambamba na Hamisi Mwesi , mfanyakazi wa Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ - Mazao) ( Mzinga) baada ya kutunukiwa Shahada ya kwanza ya Sanaa na Mawasiliano ya Umma kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro ( MUM) Hajjat Mwatumu Malale ( hayupo pichani) Novemba 17, mwaka huu katika viwanja vya Chuo Kikuu hicho.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya kwanza la ualimu.
Baadhi ya wanachuo wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro wakifuatilia hotuba.Picha na John Nditi,Globu ya Jamii- Morogoro.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa