RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APONGEZA NSSF NA JESHI LA MAGEREZA KUKAMILISHA MRADI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI


RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN APONGEZA NSSF NA JESHI LA MAGEREZA KUKAMILISHA MRADI WA UWEKEZAJI WA KIWANDA CHA SUKARI MKULAZI

*Asema mradi huu una umuhimu wa kipekee
*Asema kiwanda hicho kinaenda kutoa uhakika wa sukari nchini, awapongeza NSSF na Jeshi la Magereza kwa kufanikisha mradi huo

Na MWANDISHI WETU,
MOROGORO. Historia imeandikwa na hakika hakuna kilichokwama! Unaweza kusema hivyo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua rasmi mradi wa kiwanda cha sukari Mkulazi, kilichopo Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro na kusema mradi huo anataka uwe endelevu kwa maslahi mapana ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Uzinduzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha sukari tani 50,000 kwa mwaka umefanyika tarehe 7 Agosti, 2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali. NSSF kupitia mradi huo imetekeleza moja ya jukumu lake la uwekezaji; majukumu mengine ni  kuandikisha wanachama wapya kutoka sekta binafsi na sekta isiyo, kukusanya michango na kulipa mafao.

Akizungumza na wananchi waliohudhuria hafla hiyo Mhe. Rais Dkt. Samia amewapongeza wana hisa wa kiwanda hicho ambao ni NSSF na Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Uzalishaji Mali (SHIMA), kwa kukamilisha mradi huo wenye manufaa makubwa na kuwa Serikali inafanya kila jitihada kutanua mradi huo.

Aidha, amepongeza mradi huo kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania pamoja na wakulima kupata soko la uhakika wa kuuza miwa. Pamoja na hilo amepongeza mradi huo kutumia umeme ambao unaozalishwa kiwandani hapo.  Amesema dhamira na malengo ya Serikali ni kuhakikisha mradi huo unakua na kuleta tija kubwa kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema ujenzi wa kiwanda hicho unatokana na maono ya Rais Dkt. Samia ambaye aliahidi kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ukiwemo wa Mkulazi. Amesema baada ya Rais Dkt. Samia kuingia madarakani mwezi Machi 2021, aliridhia mradi huo kuendelea na kuwa unaenda kupunguza nakisi ya sukari nchini na kutatua changamoto ya ajira.

Amesema uwekezaji wa mradi huo umeongeza wigo wa kodi na umechechemua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Malima amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa ziara yake katika mkoa huo ambayo imekuwa na mafanikio makubwa hasa katika kuzindua miradi ya kimkakati ukiwemo wa kiwanda cha sukari Mkulazi ambao umetoa fursa nyingi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akitoa taarifa ya mradi wa kiwanda hicho, Dkt. Hildelitha Msita, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mkulazi, amesema wataendelea kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuondoa nakisi ya sukari nchini pamoja na kuongeza ajira kwa Watanzania kwa kusimamia uendeshaji wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kuzalisha tani 50,000 za sukari kwa mwaka na tayari uzalishaji wa sukari ya majumbani ulianza tarehe 1 Julai, 2024 ambapo kwa siku kinazalisha tani 250.

Kwa upande wake Mhandisi Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amesema mradi huo umekuwa na faida kwa Jeshi la Magereza na kuwa faida hizo zinatokana na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia kuhakikisha wanatumia vizuri rasilimali za Jeshi hilo kwa kuleta tija na kutoa mchango kwa jamii na Taifa.

Naye Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amesema uwepo wa mradi wa kiwanda hicho unatoa fursa mbalimbali kwa wananchi, hivyo watahakikisha kiwanda hicho kinazalisha sukari ya majumbani na viwandani na kinalindwa kwa maslahi mapana ya Taifa.

Aidha, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Viwanda na Biashara, amesema Serikali ya awamu ya sita imeweka historia kubwa ikiwemo kuongeza idadi ya viwanda takribani 18,000 ndani ya miaka mitatu.

Mbunge wa Jimbo la Kilosa, Profesa Kalamagamba Kabudi amesema wananchi wa jimbo hilo wanashukuru ujio wa kiwanda hicho ambacho kinawasaidia kupata ajira na kupata soko la uhakika la kuuza miwa yao.



Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan afungua Daraja la Berega, Kilosa Mkoani Morogoro


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi Daraja la Berega lililopo Wilayani Kilosa katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.

Warsha ya Kitaifa Kujadili Shabaha za Kuondoa Uharibifu wa Ardhi na Mbinu Shirikishi ya Tathmini ya Ardhi (ILAM) Yafanyika Morogoro



Warsha ya Kitaifa Kujadili Shabaha za Kuondoa Uharibifu wa Ardhi na Mbinu Shirikishi za Tathmini ya Ardhi (ILAM) Yafanyika Morogoro

Wataalamu na wadau wa sekta mbalimbali nchini walishiriki katika warsha ya siku mbili kwa ajili ya wajumbe wa Kitaifa wa Shabaha za Kuondoa Uharibifu wa Ardhi (Land Degradation Neutrality National Working Group – LDN WG) sambamba na mafunzo ya Mbinu Shirikishi za Tathmini ya Ardhi (Integrated Land Assessment Methodology – ILAM).

Akifungua warsha hiyo iliyoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia mradi wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Miombo ya Nyanda Kame Tanzania jijini Morogoro, Dkt. Deogratius Paulo, Mkurugenzi Msaidizi-Ofisi ya Makamu wa Rais, aliwataka wataalamu na wadau hao kuhakikisha kuwa warsha hiyo inakuwa chachu ya kufanikisha shughuli za utekelezaji wa mradi sambamba na juhudi za kitaifa na kimataifa za kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.


“Ninafahamu kwamba warsha hii imewakutanisha pamoja wataalam kutoka wizara za kisekta, taasisi za serikali, mamlaka za serikali za mitaa, washiriki wa maendeleo, asasi zisizo za kiserikali na sekta binafsi. Nyinyi ni miongoni mwa wataalam wachache ambao tunatarajia kuwa mabalozi wa kufuatilia shabaha za kupambana na uharibifu wa ardhi katika sekta zenu, huku mkiangalia mbinu za usimamizi shirikishi za kuondoa uharibifu wa ardhi.

Ni dhahiri kuwa tusipofanya kazi kwa ushirikiano kama ambavyo tumeitwa hapa, tutashindwa kufanikiwa. Hivyo, niwaite nyie kuwa 'you’re the champions of LDN na ILAM,' mabalozi wa utekelezaji wa shabaha za kupambana na uharibifu wa ardhi na hivyo kunusuru nchi yetu na ukame na jangwa,” alisema Dkt. Paulo.


Awali, Mratibu wa Mradi na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi – TFS, Zainabu Shabani Bungwa, akisoma hotuba kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi, Prof. Dos Santos Silayo, alitoa shukrani kwa Shirika la FAO na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa ushirikiano wao katika kutekeleza mradi huu, ambao unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira ya Dunia (GEF).

“Lengo kuu la mradi ni kukomesha na kubadili mwelekeo mbaya wa uharibifu wa ardhi na upotevu wa bioanuwai katika maeneo yaliyoharibiwa ya misitu ya miombo kusini-magharibi mwa Tanzania. Utatekelezwa katika maeneo ya Tabora (Kaliua Landscape) katika Wilaya za Kaliua, Urambo na Sikonge; Katavi (Mlele Landscape) kwa thamani ya dola za Marekani milioni 6.875, sawa na shilingi bilioni 16.8, kwa kipindi cha miaka mitano (2022-2027),” alisema Kamishna Msaidizi huyo.

Aliongeza kuwa moja ya shughuli za mradi huo ni kujenga uwezo wa wataalam na sekta mbalimbali katika masuala ya usimamizi shirikishi ili kuhakikisha huduma za kiokolojia kutoka katika Misitu ya Miombo zainaimarika. Alisisitiza kuwa mradi huu tutapiwa kwa uzalishaji bora wa asali na mnyororo wa thamani wa mazao ya nyuki na mengine ya kilimo.

Aidha, watalam watawezeshwa pia tathmini ya rasilimali za misitu, na manunuzi ya baadhi ya vitendea kazi katika maeneo yao. Huku akizitaja shughuli nyingine kuwa ni urejeshwaji wa ardhi iliyoathiriwa, mipango shirikishi ya matumizi bora ya ardhi, ujenzi wa vituo vya ulinzi wa misitu (ranger posts), Vituo vya kukusanya na kuchakata asali, nyumba za kufugia nyuki (bee cages) na kuwezesha upatikanaji wa vyanzo vya maji na vituo vya utunzaji wa mbegu za miti na kilimo.

Kwa kumalizia, Kamishna Msaidizi Bungwa aliwashukuru wote waliowezesha kikao hicho na kuhimiza kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha uhifadhi wa misitu, ufugaji wa nyuki, na utalii.

Warsha hiyo ilihudhuriwa na wajumbe wapatao 40.

 

NSSF MABINGWA TAMASHA LA PASAKA 2018

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanamichezo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.
Wanamichezo kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakipokelewa na wenzao wa NSSF katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kuwasili katika michezo ya tamasha la Pasaka.
 Mapokezi.
Ofisa wa NSSF, Pili Mogella (kulia), akimkaribisha Ofisa wa ZSSF.  
 ZSSF wakiwasili bandarini.
 Wachezaji wa ZSSF wakiwa ndani ya basi.
Kocha wa timu ya netiboli ya NSSF, Joseph Ngánza akitoa maelekezo kwa wachezaji wake. 
 Kocha wa timu ya ZSSF, Hadia Ahmada, akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro, akikagua timu ya netiboli ya ZSSF.
Meneja Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro akikagua timu ya netiboli ya NSSF.
 Kikosi cha timu ya ZSSF.
Kikosi cha NSSF.
Mshambuliaji wa timu ya netiboli ya ZSSF, Mwasiti Vita, akiwa katika harakati za kufunga huku Amina Jumanne (kushoto), wa NSSF akijaribu kumzuia katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Mchezaji wa NSSF, Maliti, akimiliki mpira huku akizongwa na mchezaji wa ZSSF, Yasinta (GD).
 Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akichuana na mchezaji wa ZSSF, Fatuma Sule (kushoto).
  Mchezaji wa timu ya netiboli ya NSSF, Fatuma Sule (C), akimiliki mpira.
 Timu ya netiboli ya NSSF wakiwa katika mazoezi.
Meneja wa Mahusiano na Masoko wa NSSF, Salim Kimaro (kulia), akizungumza na wachezaji kabla ya kuanza kwa mchezo wa netiboli ya ZSSF.
 Timu ya NSSF ikiwa mapumziko.
Mashabiki wa timu ya netiboli ya NSSF. 
 Wachezaji wa ZSSF wakiwa katika mazoezi
 Kocha wa timu ya soka ya NSFF, Sanifu Lazaro.
Zawadi za washindi.
Mshambuliaji wa NSSF, Katunguja, akimtoka Rashid Suleiman wa ZSSF (kulia).
Shaban Enzi (kulia), akichuana na Ismail Hubi wa ZSSF.
Ally Chuo wa NSSF (chini), akichuana na Rajabu Said wa ZSSF.
Wachezaji wa NSSF wakishangilia bao la pili la timu hiyo.
Mchezaji wa ZSSF, Seif Hafidh (kulia), akichuana na Said Mwinyi wa NSSF.
 Nahodha wa timu ya netiboli ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Pili Mogella, akipokea kombe la Ubingwa wa michuano ya tamasha la Pasaka kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete (kushoto), baada ya kuifunga ZSSF magoli 23-19  katika mchezo ulifanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akimkabidhi kombe nahodha wa timu ya soka ya NSSF, Mzee Mfaume, baada ya kuwafunga ZSSF mabao 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 Wachezaji wa timu ya soka ya NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dominick Mbwete (kushoto), akipokea zawadi ya mlango kutoka kwa Kaimu Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala wa ZSSF, Abdallah Mbwana.
Maofisa wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.
Maofisa wa NSSF na wale wa ZSSF wakiwa katika picha ya pamoja katika bandari ya Dar es Salaam baada ya kumaliza ziara ya michezo ya tamasha la Pasaka.
 
TIMU ya soka ya Shirika la Taifa ya Hifadhi ya Jamii (NSSF), imeichapa bila huruma timu ya soka ya ZSSF 2-0 katika mchezo wa tamasha la Pasaka.

Mchezo huo ulifanyika mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kwa kuzikutanisha timu mbili za mashirika ya Hifadhi ya Jamii ya NSSF na ZSSF ambapo lengo la michizo hiyo ni kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya mashirika hayo mawili.

Mchezo huo uliianza kwa kasi kubwa iliwachukua dakika 4 NSSF kujipatia bao la kwanza baada ya mwamuzi wa mchezo huo Fikiri Yusuph kutoa Penalti baada ya beki wa ZSSF kuunawa mpira katika harakati za kuokoa, mshambuliaji wa NSSF Said Mwinyi aliipiga penalti hiyo na kuipatia timu yake bao la kwanza.


Kuingia kwa bao hilo la mapema kuliwafanya ZSSF kucharuka na katika dakika ya 10 nusura wajipatie bao la kusawazisha baada ya shuti kali lililopigwa na Juma Mbwana kugonga mwamba na kuokolewa na walinzi wa timu ya NSSF.

ZSSF waliendelea kulisakama lango la NSSF lakini walinzi wa timu ya NSSF wamkiongozwa na beki wa wa timu hiyo Hemed Kagobe waliweza kuondoa hatari hizo na kuwapa wakati mgumu washambuliaji wa timu ya ZSSF.

Katika dakika ya 27 ya mchezo nusura ZSSF wapate bao la kusawazisha lakini golikipa wa NSSF, Sadick aliweza kuokoa kiki iliyopigwa na Rashid Suleimani na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Time hizo zilirndelea kushambuliana kea zamu hadi mapumziko NSSF ilitoka ikiwa inaongoza 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo ZSSF waliwatoa, Hassani Omar, Abasi Yahaya Abasi, Maulid Suleiman na Hamis Thani na nafsa zao kuchukuliwa na Yusuf Said, Abdulkarim Rajabu, Khamis Haji na Mohamed haji Khamis. 

NSSF waliwatoa Nassoro Nassor, Ally Chuo, mfungaji wa bao la kwanza Said Mwinyi, Sadick Jongo na nafasi zao kuchukuliwa na Bakari Becco, Mwinyi Mzee, Prosper Lyoba na Shaban Enzi.

Mabadiliko hayo yalibadilisha sura ya mchezo katika dakika ya 82 mshambuliaji wa timu ya NSSF, Katunguja aliifungia timu ya bao la pili banda ya kupokea pasi kutoka kwa  Mwinyi Mzee aliyeingia kipindi cha pili, kuingia kwa bao hilo kuliongeza kasi ya mchezo ambapo ZFF walikuja juu wakitaka kupata bao angalau la kufutia machozia lakini kikwazo kikubwa alikuwa mlinda mlango wa timu ya NSSF, Sadick ambaye alikuwa nyota ya mchezo kwa kuokoa mashuti yaliyokuwa yakielekezwa langoni mwake.

Wakati huohuo katika mchezo wa netiboli timu ya NSSF ilingára vilivyo baada ya kuichapa ZSSF kwa jumla ya magoli 23-19 na kunyakua kombe la michuano hiyo kwa mwaka 2018.

Akizungumza wakati akitoa zawadi kwa washindi wa michezo hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa NSSF, Dominick Mbwete, alisema kuwa michezo hii imelenga kujenga ushirikiano baina ya mifuko, kuimarisha uhusiano na pamoja na kuboresha afya kwa wadu wa michezo kupitia mifuko hiyo.

“Lengo la mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka kwa kukutanisha  wanamichezo mbalimbali kutoka katika mashirika  ya ZSSF na NSSF ambapo  kushiriki kwa pamoja michezo mbalimbali pamoja na kutoa zawadi kwa wanamichezo vote walioshiriki katika tamasha hilo."

ambapo mwakani itafanyika mjini Zanzibar na kuandaliwa na ZSSF watakuwa wenyeji wa michezo hiyo Zanzib imelenga kujenga ushirikiano baina ya mifuko, kuimarisha ushirikiano baina ya ZSSF na NSSF pia imelenga kujenga ushirikiano, uhusiano baina ya wafanyakazi kutoka ZSSF pamoja na NSSF  katika kuimarisha ushirikiano.
 
 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa