*NI kamati maalum itakayochunguza athari za bonde hilo na kumpatia majibu
*Akagua maeneo mbalimbali ya bonde hilo na kuhushudia athari zaidi
Na Mwandishi Wetu
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) ameteua Kamati
maalum ambayo itaishahuri Serikali namna ya nini kifanyike katika
kushughulikia athari za bonde la Kilombero lililopo Mkoani Morogoro.
Waziri
Dk Kigwangalla amebainisha kuwa Kamati hiyo aliyoiteua, ndio
itamshahuri juu ya bonde hilo litasimamiwa vipi pamoja na namna bora ya
hatua za kuchukua ili kulinda bonde hilo ambalo lina mahitaji makubwa
ikiwemo chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stiegler’s Gorge ambako
Serikali imeamua kuweka mikakati ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha
umeme unaotarajiwa kufikia megawatts 2100 huku pia bonde hilo likiwa na
utajiri wa kuwepo na aina zaidi ya 400 ya ndege pamoja na mnyama anaina
ya Puku ama Sheshe ambaye hapatiani duniani kote zaidi ya Tanzania
pekee.
"Hii
ndio Kamati yangu, itakayonishahuri juu ya bonde ili litasimamiwa vipi.
Hii ndio Kamati ambayo itanishahuri mimi na kwamaana hiyo Serikali kwa
ujumla wake juu ya namna bora ya uhifadhi hususani katika eneo lile la
Pori tengefu.
Hapa
kuna vitu viwili vya kuzingatia: Ardhi Ohevu (Ramsar site) ambalo lina
eneo lake huku pia eneo la pori tengefu nalo kichukua nafasi kubwa
zaidi" Amesem Waziri Dk Kigwangalla wakati wa kuteua Kamati hiyo.
Kamati
hiyo inaundwa na wajumbe mbalimbali ambao wataongozwa na Mwenyekiti wa
Kamati Ndugu Andrew Napacho, Pia wajumbe ni Brig. Gen. (Mst.) Edmund
Mndolwa, Aliyekuwa Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es
Salaam, Kamishna Mstaafu, Suleiman Kova, Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha
wafugaji Bwana Semkae Kilonzo (Policy Forum).
Wengine
ni Dk. Simon Mduma, Prof. Jaffar Kideghesho, Ruzika Muheto, Mkuu wa
Wilaya ya Ulanga, MKuu wa Wilaya ya Kilombero na Mkuu wa Wilaya ya
Malinyi.
Wemgine ni Mwenyekiti Halmashauri Ulanga, M/Halmashauri Kilombero, M/Halmashauri Malinyi na M/Halmashauri Ifakara.
Pia
yupo Mtendaji Mkuu wa KPL, Mtendaji MKuu wa Illovo, Mkuu Kikosi JKT
Chita. Wengine ni Dk. Aggrey Mlimuka, Mwakilishi kutoka mamlaka ya maji
Bonde la Kilombero, Mwakilishi kutoka Wizara ya ardhi.
Wajumbe
wengine ni Ndugu. Innocent Kylogeris, Dk. James Wakibara pamoja na
Mkurugenzi Mkuu TAWA ambaye atakuwa Katibu wa Kamati hiyo.
Hatua
hiyo inafuatia Waziri Dk Kigwangalla kufanya ziara maalum kwenye bonde
hilo la kilombero ambapo ameweza kushuhudia athari kubwa zaidi
zilizofanywa na wavamizi wakiwemo wakulima na wafugaji ambao wameonekana
kuvamia maeneo makubwa ndani ya pori tengefu la bonde pamoja na Kwenye
eneo ohevu ndani ya bonde hilo.
0 comments:
Post a Comment