Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Sayansi ya wanyama ,ukuzaji viumbe maji na nyanda za malisho , Dk Nazael Madalla ( mwenye kuvaa miguuni mabuti ya mvua ) kuhusu mashine ya kusaga majani ya malisho ya mifugo hasa ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza ufugaji wa kisasa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017 na ( watano kutoka kulia ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiangalia aina ya majani ya malisho yaliyosagwa na mashine kwa ajili ya kulisha ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza ufugaji wa kisasa na malisho katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017 na ( kushoto kwake ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiwapatia ng’ ombe wa maziwa majani ya malisho yaliyosagwa na mashine wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza ufugaji wa kisasa katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017 na ( kushoto ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .( Habari na Picha na John Nditi).
Na John Nditi, Morogoro
UONGOZI
wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umeingia makubaliano ya
pamoja na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne , Dk Jakaya Kikwete
ili kulitumia shamba lake la mifugo lililipo kijijini kwake Msoga ,
liwe shamba darasa la kutolea elimu ya vitendo kwa wanafunzi wao ,
wataalamu wa mifugo na wafugaji.
Makamu
Mkuu wa SUA , Profesa Raphael Chibunda alisema hayo Nov 20, 2017
wakati Rais Mstaafu Kikwete alipofanya ziara ya siku moja na
wataalamu wake wa Mifugo walipofika Chuoni hapo kwa ajili ya kujifunza
kuhusu ufugaji bora wa Ng’ombe wa maziwa.
Rais
Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji wa
kisasa wa ng’ombe wa maziwa , kilimo cha mazao ya chakula na matunda
hasa mananasi kijijiji Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo , mkoa wa
Pwani.
“
Tumemwomba Rais Mstaafu Kikwete lile shamba lake la mifugo tulitumie
kuwa ni shamba darasa kwa wanafunzi wetu wa Sanyansi ya wanyama ,
ukuzaji viumbe majini na Nyanda za Malisho pamoja na wataalamu wa mifugo
na wananchi hasa wafugaji” alisema Profesa Chibunda na kuongeza .
“ Katika ombi letu naye ameridhia shamba hilo litumike kuwa shamba darasa” alisema Profesa Chibunda.Makamu
mkuu wa Chuo hicho alisema , kwa kuridhia kwake , SUA inaweza kusongeza
elimu bora ya ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa na nyama na
matumizi ya malisho bora kwa wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya
karibu na nje badala ya mtu mmoja mmoja kufika Chuoni hapo.
Kwa
upande Rais Mstaafu alisema “ Nimefuata kujifunza na nimelizika na
nilichokifuata na nimekipata na ahadi yangu kwenu SUA nitaendeela
kushirikiana nayi , lengo ni kuleta mabadiliko ya kisayansi ya sekta
ya ufugaji iweze kumletea tija mfugaji” alisema Rais Mstaafu Kikwete.
Naye
Naibu makamu mkuu wa chuo hicho , Profesa Peter Gilla alisema, Sua
itaendelea kufanya tafiti mbalimbali kwenye sekta ya Kilimo na Mifugo
na kupanua wigo wa uzalishaji mkubwa wa mbegu za aina mbalimbali
zikiwemo za matunda kwa nia ya kimaabara ya uhandisijeni ili kuwezesha
mahitaji katika soko la Dunia.
0 comments:
Post a Comment