Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi
ya Ardhi Bi. Albina Burra, akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi hiyo Dkt. Stephen Nindi
Wadau
mbalimbali wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra wakati akitoa maneno ya utangulizi
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya
Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi. Albina Burra akiwasilisha mada juu ya Sera,Sheria, Miongozo na Uratibu katika upangaji,utekelezaji
na usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Bi
Tabu Njonde akiuliza swali na kutaka kujua migogoro kati ya kijiji na kijiji
ina adhari gani na namna gani wanaweza kuepukana nayo.
Afisa
Mtendaji wa Kijiji cha Katurukila Bw. Salumu Lubala akiuliza swali juu ya
Umilikishwaji wa Ardhi.
Afisa
Mipango Miji kutoka wilaya ya Kilombero Bw. Remigi Lipiki akijibu maswali
mbalimbali yaliyoulizwa na wadau wakati wa warsha hiyo.
Afisa
Ardhi Mteule kutoka Kilombero Bi. Syabumi Mwaipopo akijibu maswali mbalimbali
yaliyoulizwa na wadau wakati wa warsha hiyo.
Afisa
Mipango kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Gerald
Mwakipesile akitoa tathimini ya tafiti iliyofanywa na wataalamu kutoka Tume wakishirikiana
na African Wildlife Foundation ambayo ilionesha hali halisi ya usimamizi wa
mipango ya Ardhi katika ukanda wa Udzungwa,Magombera na Selous,utunzaji wa
Mazingira na Bioanuai,Mipango ya matumizi ya Ardhi na hati miliki za kimila na
migogoro ya ardhi.
Wadau mbalimbali wakimsikiliza Bw. Mwakipesile
akiwasilisha mada
Afisa
Mtendaji wa Kata ya Mkula Bw. Christopher Kafunga akitaka kupata ufafanuzi kuhusu kupata mkopo wa fedha kutoka Benki kwa
kutumia hati miliki ya ardhi.
Diwani
wa Kata ya Msolwa Station Mh. Hakim Songa akiuliza maswali kuhusiana na maswala
ya ardhi na umilikishwaji
Afisa
uhifadhi na usimamizi wa Mazingira na usafi kutoka Wilaya ya Kilombero Bw.
Samwel Mtafya akijibu maswali mbalimbali yaliyohusu mazingira.
Msaidizi
wa Misitu Mwandamizi kutoka Wilaya ya Kilombero Bw. Peter Nkunga akijibu
maswali mbalimbali yaliyohusu maswala ya maliasili.
Bi Maria Sengelela Afisa Miradi wa asasi ya kiraia ya
Solidardad akielezea jinsi wanavyoshirikiana na Tume ya Taifa ya Mipango ya
Matumizi ya Ardhi katika kuhimiza matumizi Bora ya Ardhi
Bw.
Eugine Cyrilo kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi akichangia
jambo kuhusiana na maswala ya mazingira
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bi.
Albina Burra akitoa neon la kufunga warsha hiyo.
Diwani wa Kata ya Mang'ula Mh. John Mjami akitoa neno la shukurani baada ya kumalizika kwa warsha hiyo na kusema kuwa imewasaidia kupata majibu ya kwenda kuwapatia wananchi wao na kuendelea kuwapa elimu zaidi juu ya usimamizi wa matumizi ya Ardhi,uhifadhi wa Mazingira na Bioanuai.
Wajumbe wakiendelea kufuatilia warsha hiyo iliyofanyika Mang'ula Kilombero
Picha ya pamoja
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa Tanzania
Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya ardhi (NLUPC) imewasilisha Taarifa ya tathimini na kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya umiliki wa Ardhi,mipango ya matumizi ya ardhi na hifadhi ya mazingira, utafiti uliofanywa na wataalam
kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi kwa kushirikiana na
African Wildlife Foundation.
Akizungumza
na wadau wa mpango wa matumizi ya Ardhi kutoka kata za Mkula, Mang’ula, Msolwa
Stesheni pamoja na Sanje Bi. Albina Burra
alieleza kuwa Tume hiyo
inamalengo ambayo ni kuhakikisha kuwa kunatayarishwa na kunatekelezwa mipango
shirikishi ya matumizi ya ardhi kwa minajili ya usawa wa usalama wa miliki za
Ardhi, kuongeza uzalishaji wa Ardhi, uhifadhi wa mazingira na Bioanuai.
Alisema
kuwa Kilombero ni wilaya Muhimu sana katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ipo
katika ukanda wa mradi mkubwa wa Taifa wa kuimarisha kilimo wa SAGCOT pia ina wingi wa
lasirimali nyingi za Ardhi na mazingira zikiwemo za wanyamapori,ardhi yenye
rotuba,misitu,vyanzo vya maji,Bonde kubwa la Afrika ambalo lina mito mitatu
ambayo ni Ruaha,Rufiji na Ruevu, Milima ya Udzungwa, Hifadhi ya Taifa ya
Udzungwa Reserve.
“Utafiti
fiti huu ulifanywa na wataalamu kutoka tume wakishirikiana na watu wa African
Wildlife Foundation na walihusisha kanda mbili kwanza kuna Udzungwa,Magombela
na Selous kanda ya pili ni Korido ya Mgeta” Alisema Burra. Na kwamba
wamewashirikisha wadau hao kwa kuwa na wao wanafanya tafiti zinazofanana ili
kuwepo na uhusishwaji wa sekta hizi kwa ajili ya uboreshaji wa kufanya kazi
bila kuleta Migongano na athari za kimazingira.
Aliongeza
kuwa warsha hiyo ni muhimu kwa kuwa wajumbe walipata tathmini juu ya
umilikishwaji wa ardhi na kuona kama vijiji vyote vinamipango ya matumizi bora
ya ardhi na pia kuona kama vijiji vina vina hati za Kijiji na wakazi wangapi wana hati
za Kimila.
Mwisho
alizungumzia kuhusu Sera,Sheria, Miongozo na Uratibu katika
upangaji,utekelezaji na usimamizi wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Warsha hiyo ilihusisha ukanda wa Magombera-Udzungwa-Selous ,kulikuwa na kata nne ambazo ni Msolwa Stesheni,Nkula, Mang'ula B na sanje pia kulikuwa na vijiji nane vya Msolwa Stesheni,Nkula,Sonjo,Msufini,Katurukila,Kanjenja, Magombera na Sanje.
Washiriki katika warsha hiyo walikuwa ni Madiwani, ma Afisa Tarafa,Watendaji wa Kata,Maafisa watendaji wa Vijiji,Wenyeviti wa Vijiji, na wajumbe wa Serikali za Vijiji.
0 comments:
Post a Comment