Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi
Ramo Makani (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya kikazi katika eneo la Jumuiya
ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Wami Mbiki/Ushoroba mkoani Morogoro ambayo iliyolenga
kubaini changamoto mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna
bora ya kukabiliana nazo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi
Ramo Makani (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS),
Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) wakiongoza Wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kupanda mlima katika Hifadhi ya
Mazingira Asilia Uluguru mkoani Morogoro wakati wa ziara yao iliyolenga kubaini changamoto
mbalimbali za uhifadhi kwa ajili ya kuishauri Serikali namna bora ya kukabiliana
nazo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akizungumza na Wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii wakati wa ziara yao ya
kikazi katika Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru mkoani.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia
Uluguru, Cathbert Mafupa (kushoto) akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kuhusu Hifadhi hiyo.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,
Maliasili na Utalii, Mary Chatanda (wa tatu kushoto) akizungumza kutaka
ufafanuzi wa baadhi ya mambo kuhusu Hifadhi ya Mazingira Asilia Uluguru wakati
wa ziara ya kamati kwenye hifadhi hiyo. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo
Makani (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhandisi Atashasta Ndetiye (wa
nne kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos
Silayo (wa pili kulia).
0 comments:
Post a Comment