Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Afisa
kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana Haruna
Kiyungi akieleza jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji kodi ya pango la
ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki
Afisa
Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Bwana David Malisa (katikati) akitoa
mafunzo kwa Maafisa kutoka Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Ardhi kanda ya
Ziwa jinsi ya kutumia Mfumo wa GePG
Afisa
kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi Joines
Mhalila akielekeza jinsi ya kutumia simu katika kufanya malipo ya kodi
ya ardhi.
Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bwana
Haruna Kiyungi akionesha kwa vitendo jinsi ya kutumia Mfumo wa ulipaji
kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi/kielektroniki.
Na. Hassan Mabuye
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ikishirikiana na Wizara ya
Fedha, imesambaza maafisa wake katika halmashauri 169 kote nchini.
Maafisa
hawa wanaotoa mafunzo katika vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi
na tozo nyingine kwa kutumia simu ya mkononi ili kuondoa kabisa mfumo
wa zamani wa malipo.
Zaidi
ya maafisa 170 kutoka makao makuu ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya Fedha
na kutoka kanda nane za ardhi wameanza kutoa elimu hiyo katika
halmashauri na vituo vyote vya makusanyo ya kodi ya ardhi ili
kurahisisha ulipaji kodi ya ardhi kwa wananchi kwa kutumia simu zao na
kuondoa usumbufu.
Mfumo
wa ulipaji kodi ya pango la ardhi kwa njia ya simu ya mkononi ni mfumo
wa kielektroniki wa Government electronic Payment Gateway (GePG) katika
makusanyo ya kodi ya pango la ardhi ambao utamrahisishia mwananchi
kulipia popote walipo kwa kutumia simu zao kwa urahisi zaidi.
Mwananchi
yeyote anayemiliki kiwanja au shamba lililopimwa na kupatiwa hati,
ataweza kutumia simu yake ya mkononi kujua kiasi cha kodi ya pango la
ardhi anachodaiwa na kukulipa kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Ili
kujua unadaiwa kiasi gani cha kodi ya pango la ardhi kwa kutumia simu
ya mkononi bonyeza *152*00# au kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi
yaani sms halafu unatuma kwenda namba 15200 na baada hapo unaweza
kulipia kwa njia ya Mpesa, Tigo Pesa au kulipia tawi lolote la benki ya
NMB na CRDB.
Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza rasmi kutumia mfumo huu
wa kielektroniki wa GePG katika makusanyo ya kodi ya pango la ardhi
pamoja na tozo nyingine zinazotokana na sekta ya ardhi nchini na kuondoa
kabisa mfumo wa zamani.
Mfumo
huu utamrahisishia mwananchi kulipa kodi ya pango la ardhi popote
alipo, ikiwa ni pamoja na kulipia tozo nyingine mbalimbali za sekta ya
ardhi. Mmiliki wa kipande cha ardhi ataweza kujua anadaiwa kiasi gani
cha kodi ya pango la ardhi na kulipia popote alipo bila kusumbuka
kufuata huduma hizo katika vituo vya makusanyo.
Kwa
majaribio ya ukusanyaji kodi ya pango la ardhi kwa kutumia mfumo wa
kielektroniki yalifanywa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani na baada
ya mafanikio makubwa kuonekana elimu ikatolewa kwa watendaji wote wa
sekta ya ardhi katika Halmashauri zote za mkoa wa Dar es salaam kabla ya
zoezi hilo kuhamishiwa mikoani.
Kwa
zile huduma nyingine za sekta ya ardhi ambazo zinahusisha malipo kama
vile upekuzi katika daftari la msajili (official search), mwananchi
atapaswa kutembelea ofisi za Wizara ya ardhi zilizo katika eneo lake na
kupatiwa makadirio ya kulipia huduma husika pamoja na namba ya malipo
itakayomuwezesha kulipia aidha kwa njia ya benki au simu ya mkononi.
Kwa
sasa kikosi kazi kinachotoa mafunzo juu ya matumizi ya mfumo huu
kimeshaanza kuelemisha mikoa mingine baada ya kupata mafanikio mazuri
katika mkoa wa Dar es Salaam. Lengo kubwa la kutumia mfumo huu ni
kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa maduhuli ya serikali pamoja na
kurahisisha ulipaji kodi ya pango la ardhi nchini.
0 comments:
Post a Comment