NA Beatrice Lyimo-MAELEZO
Dar es Salaam.
Serikali
imeunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka wizara sita zinazoshukulika
na masuala ya ardhi ili kuweza kutafuta ufumbuzi wa kudumu katika
kutatua changamoto mbali mbali za ardhi ikiwemo maeneo ya Hifadhi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaamu Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani alisema kuwa lengo la kuhusisha
Wizara hizo ni kufanya uchunguzi wa kina na wa kisheria kuhusu namna
bora na endelevu ya kumaliza changamoto katika sekta ya ardhi.
“Serikali
imeamua kuunda kikosi kazi chenye wajumbe kutoka Wizara ya Ardhi ikiwa
ni wadau wakuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu
TAMISEMI, Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji na Umwagiliaji
pamoja na Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo kwa madhumuni mapana
ya kufanya uchunguzi wa kina na kupitia sheria zote endelevu za kumaliza
changamoto za ardhi inayohusisha maeneo ya hifadhi” alifafanua Mhandisi
Kamani
Mhandisi
Makani alisema kuwa kikosi hicho kimeanza kufanya kazi ya kusoma
taarifa mbalimbali za baadhi ya maeneo yenye changamoto za ardhi na hivi
karibuni kinatarajia kutembelea maeneo hayo ili kujua chanzo cha
matatizo na jinsi ya kushughulikia changamoto hizo.
Aidha,
katika hatua hiyo ya Serikali ya kuendelea kutafuta ufumbuzi wa kudumu
na endelevu wa changamoto za ardhi, Mhandisi Makani amewataka viongozi
na watumishi wanaohusika na zoezi hilo kuzingatia taratibu katika
kutekeleza sheria kwa wananchi walioko katika vitongoji na vijiji
vilivyosajiliwa.
Vilevile
Mhandisi Makani amewataka wananchi walioko katika maeneo hayo
kutoanzisha shughuli mpya za kibinadamu na kutoendelea na shughuli za
kibinadamu zinazosababisha uharibifu wa mazingira na kuathiri tabia
nchi.
Wakati huohuo
Mhandisi Kamani amewataka wafugaji kuondoa haraka mifugo iliyoko ndani
ya maeneo yaliyoifadhiwa kisheria kwa kuzingatia taratibu zilizopo.
Mbali
na hayo Serikali imewataka wananchi kutii sheria na kuepuka vitendo
viovu vinavyosababisha kupotea kwa uoto wa asili kwa kasi inayoendelea
nchini na kutishia uhifadhi endelevu.
0 comments:
Post a Comment