Na Beatrice Lyimo- MAELEZO
08/09/2016
Serikali imesema ni kinyume cha sheria kwa askari mgambo kuwanyanyasa Mama Lishe na wafanyabiashara wengine wadogo nchini.
Akijibu
swali la Mhe. Zaynab Vulu (Viti Maalumu) alilotaka kujua kwanini
Serikali isiandae mazingira mazuri ya kufanyia kazi wafanyabiashara hao,
Naibu Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Mhe. Seleman Jaffo
amemesema kuwa askari mgambo wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu bila kuwanyanyasa wala kuwadhulumu wakati wakiwaondoa katika
maeneo yasiyoruhusiwa.
Naibu
Waziri Jaffo aongeza kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa
wafanyabiashara hao walioko katika sekta isiyo rasmi katika kukuza
kipato na ajira.
Aidha,
Naibu Waziri Jaffo amesema kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kwa
askari mgambo yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo vya
kuwanyanyasa wafanyabiashara na Mama Lishe wanapotekeleza majukumu yao.
Mbali na hayo, Naibu Waziri amezikumbusha Halmashauri
zote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo
wakiwemo Mama Lishe karibu na maeneo walipo wateja wao.
Zaidi
ya hayo Naibu Waziri huyo amewataka wafanyabiashara wadogo nchini
kufanya biashara katika maeneo yaliyotengwa rasmi na Halmashauri na
kuacha kufanya biashara hizo katika maeneo yasiyoruhusiwa.
0 comments:
Post a Comment