KATIBU Mkuu wa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Florens Turuka
amesema Serikali iko tayari kushirikiana na watafiti wa kilimo kuandaa
mazingira yatakayowezesha nchi kuruhusu uzalishaji wa mazao yanayotokana
na Uhandisi Jeni (GMO).
Akizindua ripoti ya hali ya biashara kwa mazao ya baiteknolojia jana
mjini hapa, Dk Turuka alisema lengo la kuruhusu mazao hayo ni kufanya
kilimo kiwe na tija kubwa kutokana na sekta kukabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ukame na magonjwa.
“Tanzania hatuwezi kukwepa matumizi sahihi ya teknolojia, lazima
tuhakikishe tunakuwa na matumizi sahihi na kuondoa wasiwasi ndani ya
jamii yetu,” alisema Dk Turuka.
Alisema ipo haja ya watafiti na serikali kufanya kazi kwa karibu ili
kutoa elimu juu ya upotoshaji unaofanywa na wanaharakati kuhusu mazao ya
GMO.
Dk Turuka alisema sheria na kanuni zilizokuwepo awali zimerekebisha na sasa utafiti wa mazao ya GMO umeruhusiwa nchini.
Alisema serikali inaendelea kuandaa miongozo mbalimbali ambayo
itasimamia mazao ya baiteknolojia. Alitoa mwito kwa watafiti hao kufanya
karibu na Serikali ili kuielimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya
teknolojia ya GMO.
Chanzo Gazeti La Habari Leo
0 comments:
Post a Comment