Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SERIKALI imesema inaangalia uwezekano wa kutumia mtambo wa
satelaiti, kufikisha huduma ya mawasiliano ya simu katika maeneo korofi
nchini.
Maeneo hayo ni yaliyo kwenye changamoto za kijiografia yaliyopo
maeneo ya mabondeni na milimani, ambako watoa huduma za simu wameshindwa
kuyafikia kutokana na kutokuwa na mvuto wa kibiashara.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa
Faustin Kamuzora alisema hayo mkoani Morogoro akiwa kwenye ziara ya
ukaguzi wa minara ya simu ya Vodacom na Tigo katika kata za Kanga na
Maskati wilayani Mvomero.
Mvomero ipo katika mradi wa mawasiliano vijijini wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Ziara hiyo iliongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote (UCSAF), Peter Ulanga na wahandisi wa minara hiyo kutoka
kampuni za Tigo na Vodacom.
Profesa Kamuzora alisema ameridhishwa na kazi ya miradi hiyo baada ya
kuikagua na kubaini mawasiliano yanapatikana. Alitaka kampuni zilizo
kwenye mradi huo, kuhakikisha zinatatua changamoto ndogo zilizopo miradi
hiyo iwe endelevu.
“Inabidi sasa kuangalia suala la matumizi ya satelaiti kwa maeneo
ambayo jiografia yake ni ngumu, hasa kwa watu wanaokaa mabondeni.
Nimeridhishwa na mradi hasa kwa namna walivyoamua kutumia teknolojia ya
umeme wa jua katika minara yote,” alisema hayo akiwa kwenye mradi wa
Maskati, uliopo kilometa 110 kutoka Morogoro mjini.
CHANZO GAZETI LA HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment