Na: Lilian Lundo – Maelezo – Dodoma
Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
imetenga jumla ya shilingi Bilioni 2.5 katika bajeti ya mwaka 2016/017
ili kujenga hospitali ya Wilaya ya Morogoro.
Hayo
yamesemwa leo,Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Selemani
Jaffo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Morogoro Mjini Mhe. Azizi
Abood juu ya msongamano mkubwa wodi za akina mama hospitali ya Rufaa
Morogoro.
“Msongamano
wa wagonjwa katika wodi ya wazazi Hospitali ya Mkoa unatokana na
kukosekana kwa hospitali ya Wilaya ya Morogoro.Ili kukabiliana na tatizo
hilo, Serikali immepanga kuanza ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya
Morogoro katika bajeti ya mwaka 2016/17,” alisema Mhe. Jaffo
Mhe. Jaffo aliendelea kusema kuwa, fedha hizo zilizotengwa zitaanza kwa ujenzi wa jengo la utawala na jengo la wagonjwa wa nje.(OPD).
Aidha,
aliendelea kujibu maswali ya yaliyoelekezwa katika wizara hiyo kwa
kusema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga shilingi
milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa chumba cha kuhifadhi maiti (mortuary)
Wilaya ya Chunya.
Chumba
hicho cha kuhifadhi maiti kinatarajiwa kugharimu shilingi milioni 230
ambapo ujenzi wa jengo utagharimu shilingi milioni 60 na Majokofu
yatagharimu shilingi milioni 160.
Kwa
sasa Wilaya hiyo ina chumba maalum ambacho kimetengwa kwa ajili ya
kuhifadhi mati mbili tu ambacho hakitoshelezi huduma hiyo hali ambayo
huwalazimu wahitaji kufuata huduma ya kuhifadhi maiti Hospitali ya Mkoa
wa Mbeya.
0 comments:
Post a Comment