Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
DIWANI wa Kata ya Hembeti wilayani Mvomero kupitia Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Peter Mdidi amesema licha ya kuwa
mpinzani, anamkubali Rais John Magufuli kutokana na utendaji wake wa
kazi unaolenga kuimarisha uwajibikaji wa viongozi na watendaji katika
kuwahudumia wananchi.
Amesema anamkubali kwa asilimia 100 Rais Magufuli kutokana na falsafa
yake ya ‘Hapa Kazi Tu’, inayoendana na uchukuaji wa hatua mbalimbali za
kinidhamu kwa watendaji wa serikali wanaobainika kwenda kinyume cha
maadili na kutowajibika ipasavyo kwa wananchi.
Diwani huyo alisema hayo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba mapema wiki hii
katika kijiji cha Dihombo, kata ya Hembeti wilayani hapa.
Mwigulu alifika kijiji cha Kambara kujionea hali
baada ya mifugo 80 wakiwamo mbuzi, kondoo na ndama kukatwa mapanga na
wengi kufa na wengine kujeruhiwa.
“Mimi ingawa nipo upinzani lakini ni muumini mkubwa wa falsafa ya
Rais Dk Magufuli. Nimekubali kwa asilimia 100 ya uchapakazi wake...na
hii inatakiwa ifanyike kwa viongozi wengine wa ngazi ya wilaya hii ya
Mvomero tofauti na ilivyo sasa ambapo migogoro ya wakulima na wafugaji
bado inaendelea kutokea,” alisema.
Alimtaka Mwigulu kuwa makini na migogoro hiyo kwa kuanza kuchunguza
mwenyewe kubaini kiini chake badala ya kusikiliza taarifa za viongozi wa
ngazi ya wilaya hiyo, ili afanye maamuzi sahihi ya kumaliza migogoro
baina ya wakulima na wafugaji wilayani humo.
CHANZO: HABARI LEO.
0 comments:
Post a Comment