
Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari yapatayo matatu
Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.
Habari
kutoka Kilombero zilizothibitishwa na mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Bw.
Leph Gembe zinadai kuwa ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa 1 usiku
wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga.
Alisema
kuwa Jumla ya watu zaidi ya 30 ndio walikuwepo katika kivuko hicho na
kuwa jitihada za uokoaji zilifanyika na watu zaidi 29 waliokolewa
Alisema
chanzo cha ajali hiyo ni upepo Mkali na mawimbi makali yaliyopelekea
kivuko hicho kuzama na kuwa hadi sasa bado taarifa kamili kupatikana na
pindi atakapopata habari kamili atazitoa
Mkuu huyo alisema kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP
CHANZO MICHUZI MEDIA GROUP
0 comments:
Post a Comment