Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki
mkoani Morogoro kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Celina Ompeshi
Kombani amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu huko nchini India.
Akitoa taarifa hiyo ya msiba, Katibu wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Thomas Kashililah alisema
kuwa, marehemu Kombani alikua akisumbuliwa na maradhi ya kisukari na
shinikizo la damu hivyo alikwenda nchini India kwa ajili ya matibabu
ndipo mauti yakamkuta kule.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa leo kutoka India kuja Tanzania kwa ajili ya mazishi.
Bi. Celina Kombani alizaliwa Juni 19 mwaka 1959 na kufariki leo Septemba 24 mwaka 2015.
Mungua ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!
0 comments:
Post a Comment