Home » » OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

OFISI YA RAIS, TUME YA MIPANGO YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Mapema wiki iliyopita Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilitembelea miradi ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini ili kukagua utekelezaji wake. Miradi hiyo ni pamoja na Kituo cha kuzalisha samaki Morogoro, Skimu ya Umwagiliaji Iringa vijijini, Maghala ya COWABAMA Iringa Vijijini, Ujenzi wa Barabara ya Iringa – Dodoma, Bwawa la Mtera, Ujenzi wa Barabara ya Manyoni – Itigi, utandikaji wa Reli eneo kati ya Kitaraka na Malongwe, Shamba la Kitengule, One Stop Border Post Mutukula, Mkongo wa Taifa Mutukula na Upanuzi wa mradi wa maji safi, Bomba Kuu la Ziwa Victoria.  

Katika kufanikisha uratibu wa miradi ya maendeleo, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango hufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuzielekeza Wizara zinazotekeleza miradi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kila robo mwaka. Aidha, Tume ya Mipango hutembelea miradi ya maendeleo kuona hali halisi ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na kubaini mafanikio na changamoto na hatimaye kutoa ushauri katika ngazi husika kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

Moja ya Majukumu ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ni kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kitaifa ya Kimkakati, Miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (MMS) na miradi mingine muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Taifa. Miradi imeainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015/16) na ile ya Matokeo Makubwa Sasa iliyoibuliwa katika mfumo wa kimaabara. 

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa