Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akizindua Tawi la CCM la
Wajasiriamali Bodaboda na Mama lishe lililopo Mgulu wa Ndege Kata Ya
Mkundi Manispaa ya Morogoro.Mara Baada ya Kuzindua Tawi Hilo Mh Abood
Aliongea na Wanachama wa Tawi Hilo Kisha Kuwaelekeza Kujiunga Kwenye
Vikundi vya Wajasiriamali Yeye Atakuwa Tayari kuwawezesha Mitaji ya
Kufanya Shuguli za Kujiletea Maendeleo.
Mbunge
wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akiwa Meza Kuu Sambamba na
Katibu wa CCM Kata Ya Mkundi tayari Kusikiliza Kero zinazowakabili
wakati wa Kata Hiyo Ambapo walimwambia Wanakabiliwa na Kero Kubwa ya
Umeme,Maji na Barabara.Aidha Mh Abood Akitoa Majibu Kuhusu Kero Hizo
Alesema Kuhusu Umeme Serikali Imeiweka Kata Hiyo Kwenye Bajeti ya
Serikali ya Mwaka huu .Kuhusu Maji Mh Abood alitoa Shilingi
Milioni 11 Kwajili ya Kununua Vifaa vya Kuwezesha Kufikisha Maji katika
eneo la Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi.Pia Alitoa Shilingi Milion 2
kwajili ya Mafuta Ili Greda la Manispaa ya Morogoro Kuweza Kuchonga
Barabarfa Zote za Kata Hiyo.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mgulu wa Ndege Kata ya Mkundi Jimbo la Morogoro Mjini
Akisoma Risala yake Kwa Mbunge wa Jimbo Hilo Mh Aziz Abood.
Mmoja
wa Wakazi wa Kata ya Mkundi waliojitokeza Kwa Wingi Kwenye Ziara ya
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Akieleza Kwa msisitizo Kero Kubwa
Inayowakabili wakazi wa Kata Hiyo
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimsikiliza kwa Makini Mbunge wao
Wakazi wa Kata ya Mkundi wakimshangilia Mh Abood mara Baada ya Kutatua kero Kubw ya kata hiyo tatizo la Maji.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood Akijibu Baadhi ya Kero zinazowakabili wakazi wa Kata ya Mkundi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment