CHUO Kikuu Mzumbe kinatarajia kuwatunuku jumla ya wahitimu 3,943 katika madaraja mbalimbali kuanzia leo.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa chuo hicho,
Rainfrida Ngatunga, ilieleza mahafali katika kampasi kuu yanafanyika
leo ambako wahitimu 2,125 watatunukiwa, wanawake wakiwa 922.
Mahafali katika kampasi ya Mbeya yatafanyika Desemba 12, ambako 832 watatunukiwa, kati yao wanawake ni 444.
Shughuli za mahafali ya chuo hicho zitakamilika kampasi ya Dar es
Salaam Desemba 19, kwa wahitimu 986 kutunukiwa, wanawake wakiwa ni 473.
Kwa mujibu wa Ofisa huyo, wahitimu wa vituo vya kufundishia vya Mwanza na Tanga watahudhuria mahafali Kampasi Kuu.
Mahafali hayo yote yatahudhuriwa na Mkuu wa chuo hicho, Jaji Mstaafu
Barnabas Samatta na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Josephat Itika na
viongozi wengine.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment