Home » » TAMISEMI YAOMBWA KUSIMAMIA BAJETI

TAMISEMI YAOMBWA KUSIMAMIA BAJETI

OFISI ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imeombwa kusimamia kidete bajeti za Halmashauri za Wilaya zote sita mkoani hapa.
Nia ni kuzingatia mipango itakayosaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira katika maeneo yao na hivyo kuliepusha taifa na hatari ya kuingia kwenye majanga makubwa yanayotishia maisha ya viumbe hai wakiwamo binadamu.
Rai hiyo ilitolewa jana na wataalamu wanaojihusisha na mabadiliko ya tabia nchi kutoka katika wilaya sita mkoani hapa ambao wamekutana ili kujadili, ikiwa ni pamoja na kutafuta mbinu za kudhibiti uharibifu wa mazingira ili hatimaye waweze kutengeneza rasimu zitakazoingizwa katika mipango ya halmashauri hizo kwa ajili utekelezaji.
Walisema endapo hatua za kudhibiti uharibifu wa mazingira hazitachukuliwa mapema miaka 10 ijayo taifa litashuhudia majanga makubwa ambayo yataathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya viumbe hai ikiwa ni pamoja na binadamu.
Chanzo;Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by : Tone Media
Copyright © 2012. Morogoro Yetu - All Rights Reserved
Template Modify by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa