Home »
» Bodi ya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) yatembelea Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda
Bodi ya ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) yatembelea Eneo la Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Maji Kidunda
|
Meneja
Usimamizi, Uendeshaji na Mazingira toka Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar
es Salaam (DAWASA) Bi.Modesta Mushi akiwaonesha wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) ramani ya maeneo
yatakayoguswa na Ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunda lenye ujazo wa Mita
milioni 190, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani Morogoro.
|
|
Mkuu
wa Msafara wa Timu ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi
Mhandisi John Kirecha akitoa maelezo kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) (Hawapo pichani)kuhusu
kukamilika kwa taratibu za ulipaji fidia kwa wakazi waliopisha ujenzi wa mradi
wa bwana la Kidunda litakaloweza kutoka huduma kwa mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani na Morogoro, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi Mkoani
Morogoro.
|
|
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) Alhaji Said El-Maamry akimueleza jambo Mkuu wa Msafara wa Timu
ya Ulipaji fidia kwa Wakazi walio katika Eneo la Mradi Mhandisi John Kirecha
ikiwemo kuhakikisha taratibu hizo haziathiri maendeleo ya ujenzi wa mradi huo,ikiwamo
kuwataka wakazi wenye matatizo ya Mirathi kuyamaliza ndipo waweze kupatiwa
fidia zao.
|
|
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) Bw. Archard
Mtalemwa (katikati mwenye shati jeupe) akiwaonesha
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) Ramani ya Viwanja 1000 vilivyopimwa vya Makazi mapya eneo la Bwira juu kwa wakazi 2068
waliopisha Mradi wa ujenzi wa Bwawa la
Kidunda, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
|
|
Msimamizi
wa Kitengo cha Usimamizi na Upimaji
Ramani wa Wilaya Mkoani Morogoro Bw. Kitomaga Francis(aliyevaa Kaunda suti) akiwaeleza Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA) mgawanyiko wa matumizi
wa viwanja hivyo ikiwamo kwa ujenzi wa shule, makazi, Hospitali, Polisi, Ofisi na
huduma nyingine muhimu za jamii, wakati wa Ziara ya Bodi hiyo katika eneo la
Mradi huo Mkoani Morogoro.
|
|
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)
wakiondoka eneo la Bwira Juu , eneo lililotegwa kwa ajili ya makazi mapya kwa
wananchi waliopisha ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Kidunga, wakati wa Ziara ya
Bodi hiyo katika eneo la Mradi huo Mkoani Morogoro.
|
(Picha na Hassan Silayo)
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment