Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHANZO cha migogoro ya ardhi isiyokwisha katika vijiji mkoani
Morogoro, kimebainika kuchochewa na vijikaratasi na vibali vyenye
maagizo kutoka kwa vigogo wenye mamlaka serikalini.
vikitaka wananchi na viongozi wa vijiji kutopuuza badala yake watekeleze yaliyo kwenye vikaratasi hivyo.
Hayo yaliibuliwa mwishoni mwa wiki kwenye mafunzo ya siku tatu kuhusu
sera na sheria za ardhi kwa wenyeviti,watendaji,makundi maalumu
wakiwemo wakulima na wafugaji wa vijiji vya Kata ya Maguha na Magubike,
wilayani Kilosa yaliyoandali na asasi ya Dira Theatre Group na
Foundation for civil society .
Madai hayo yalisababisha Diwani wa Magubike, Ernest Chilolo
aliyekuwa mgeni rasmi akishirikiana na Ofisa Mtendaji kata hiyo, James
Mnghondwa, kuhamaki na kupiga marufuku kwa watendaji na wenyeviti hao
kupokea na kufuata maagizo hayo kinyume na sheria, taratibu na kanuni za
nchi husuasani ardhi.
Katika madai hayo, baadhi ya washiriki hao wakiwemo mfugaji Lethon
Mhumbuja wa Magubike na Mwenyekiti wa Inyunywe Antho Nyangasi, walisema
kutokana na kuviheshimu vikaratasi hivyo, wamejikuta maeneo yao yamejaa
migogoro isiyoisha kila kukicha.
“Unakuta mtu anakibali ‘hati’ kutoka wizarani inaonyesha amepewa
karibu nusu ya kijiji na maagizo yanamtaka Mwenyekiti
atekeleze…manafikiri tufanyeje! Ndio unakuta kunaibuka vurugu maana
wakati mwingine kapewa hadi eneo lenye huduma kama maji, shule au huduma
ya afya,”alisema Mhumbuja.
Walisema migogoro katika vijiji mkoani Morogoro inatokana na wananchi
kutoshirikishwa katika utwaaji maeneo, uwekezaji usio na tija,
vijikaratasi vitokanavyo na ubabe na nafasi walizonazo vigogo maofisini
na uelewa mdogo walionao viongozi wa vijiji na wanachi juu ya masuala ya
ardhi.
Walisema sababu nyingi ni umasikini walionao wanachi ambao umekuwa
kichocheo kikubwa cha uuzwaji ardhi bila kufuata misingi na taratibu
yenye tija kwao na jamii zinazowazunguka.
Diwani Chilolo na Mtendaji kata Mnghondwa mbali na kupiga marufuku
kupokea vijikaratasi hivyo, waliwataka viongozi hao wa vijiji kuanza
kuainisha maeneo yanayoendeshwa kinyume na sheria na shuguli tofauti,
ili wote waliohusika waburuzwe kwenye vyombo vya sheria.
Awali, Mkurugenzi wa Dira, Erasmo Tulo, aliwataka viongozi wa vijiji
hadi kata kutojishusha kwenye mamlaka waliyopewa kwa kusimamia
kikamilifu sheria, taratibu na kanuni za utumishi bila kujali katika
utekelezaji huo anayeumia ni nani.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment