TAARIFA
ZILIZOIFIKIWA GLOBU YA JAMII USIKU HUU,ZINAELEZA KUWA ALIEKUWA
MUONGOZAJI WA FILAMU NA VIPINDI MBALI MBALI VYA TELEVISHENI HAPA
NCHINI,GEORGE TYSON (PICHANI), AMEFARIKI DUNIA.
GEORGE
TYSON AMEFIKWA NA MAUTI HAYO USIKU HUU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA SANA
BAADA YA GARI WALIOLOKUWA WAKISAFIRIA KUTOKA MKOANI DODOMA KUJA DAR ES
SALAAM, KUPINDUKA MARA KADHAA KUTOKANA NA KUPASUKA MATAIRI YA GARI HIYO
AINA YA TOYOTA NOAH.
AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA MOJA JIONI,ENEO LA GAIRO MKOANI MOROGORO.WAALIKUWA WAKITOKEA KWENYE HAFLA YA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KIPINI CHA TELEVISHENI CHA THE MBONI SHOW.
NDANI
YA GARI HILO KULIKUWA NA WATU WANANE AMBAO NAO HALI ZAO NI MBAYA
KUTOKANA NA KUUMIA MAENEO MBALI MBALI YA MIILI YAO. WOTE WALIKIMBIZWA
HOSPITALI YA RUFAA YA MOROGORO KWA MATIBABU.
MAREHEMU TYSON ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WATAALAMU WALIOLETA MABADILIKO MAKUBWA KATIKA TASNIA YA FILAMU NA TV NCHINI, AKIONGOZA FILAMU NA VIPINDI VINGI VILIVYOPATA MAFANIKIO MAKUBWA. ALIKUWA MUME WA MSANII YVONNE CHERRY 'MONALISA' AMBAYE WALIPATA MTOTO WA KIKE, SONIA.

TUTAENDELEA KUPEANA TAARIFA KADRI ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA.
GLOBU YA JAMII INAUNGANA NA NDUGU, JAMAA NA MARFIKI WA MAREHEMU GEORGE TYSON KATIKA KUOMBOLEZA MSIBA HUU.
MOLA NA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMIN.
MOLA NA AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMIN.
0 comments:
Post a Comment