Said Amanzi
Akitoa maamuzi hayo baada ya madiwani kukaa kama kamati na kupitia hoja mbalimbali, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Kibena Kingo alisema baraza hilo limeamua hayo baada ya watumishi hao kati ya watumishi waliofukuzwa kazi mwaka jana kuamua kukata rufaa mahakamani na mahakama kuamuru warudishwe kazini.
Kingo alisema baada ya kufuatilia kwa kina watumishi hao walikutwa na makosa ambapo mmoja alikutwa na hatia ya kutoa fedha kiasi cha Sh. milioni10 bila kufuata sheria na taratibu za uhasibu na kwamba baraza liliazimia kumshusha daraja moja la mshahara pamoja na kurejesha fedha hizo kwa muda wa miezi sita.
Aidha mtumishi mwingine anadaiwa alihusika kuweka sahihi kwenye cheki mbili tofauti ambapo fedha hizo hazikufanya kazi iliyokusudiwa.
Mwenyekiti huyo aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kusimamia nafasi zao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea huku wakitambua kuwa wananchi wanataka mabadiliko hivyo wafanye kazi kwa uadilifu.
Akizungumzia tatizo la ukusanyaji mapato, Kingo alisema kuna udhaifu mkubwa katika sula hilo hivyo aliwata watendaji kuhakikisha wanarudisha vitabu vya zamani vya ukusanyaji mapato ili waweze kuchukua vipya.
Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Said Amanzi aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi jambo ambalo litawasaidia kufanya kazi kwa bidii.
Aidha aliwasisitizia kuacha tabia ya kusubiri kufukuzana kazi akisema hali hiyo inapotokea serikali ndio inayobeba mzigo wa kumgharimia mtumishi aliyefukuzwa hivyo aliwataka kujenga tabia ya kuonyana mara kwa mara kuliko kukimbilia kufukuzana kazi.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment