TRENI
ya mizigo iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda mkoani Kigoma,
imeanguka mkoani Morogoro ikiwa na mabehewa 13 ambayo yameharibika
vibaya.
Chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu iliyotokea katika injini
wakati treni hiyo ikiwa safarini na kusababisha irudi nyuma kwa kasi.
Akizungumzia
tukio hilo, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo, John
Wariko alisema treni hiyo yenye kichwa namba 8906, ilianguka Februari 16
mwaka huu, saa 12 asubuhi katikati ya Stesheni ya Ngerengere na
Kinonko, wilayani Morogoro.
"Mabehewa sita yalikuwa yamebeba mafuta aina ya petroli mengine yalibeba bidhaa mchanganyiko ambazo ni chumvi, ngano na saruji.
"Ni
mapema mno kwa sasa kugundua hasara iliyopatikana kutokana na treni
hiyo kuanguka porini hadi mizigo yote ipakuliwe tujue iliyosalimika ni
ipi," alisema.
Kwa upande wake, dereva wa treni hiyo aliyefahamika
kwa jina la Bw. Allen Mlowe, alisema kompresa iliharibika ghafla na
treni kuishiwa upepo hali iliyosababisha mabehewa kukosa breki na kuanza
kurudi nyuma kwa kasi hatimaye kuanguka.
Alisema katika ajali hiyo alipata majeraha kidogo ya michubuko kutokana na msukosuko aliopata," alisema.
Chanzo;majira
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment