Kilombero. Wananchi wanaoishi vijiji vya Kata
ya Utengule, Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro, wamesema kuna hofu ya
kuibuka kwa mapigano baina yao na wafugaji, kutokana na viongozi
kuendekeza rushwa.
Wakizungumza kwenye Kijiji cha Mpanga juzi,
Mwinuka Kahame na Didram Nuhenga walisema viongozi hao wa Serikali hivi
sasa wamegeuza ardhi za vijiji kuwa mtaji wao.
Kahame alisema viongozi hao wanauza ardhi kwa
wageni ambayo ni mapori ya vijiji, mashamba na viwanja vya makazi huku
wakirejesha kwa kasi wimbi la wafugaji.
“Sasa hivi viongozi wanauza mapori ya vijiji,
mashamba na makazi ya wenyeji bila huruma, hawafuati taratibu wala
sheria… hakuna mikutano ya kisheria inayoitishwa,” alisema Kahame na
kuongeza:
“Wanajua wananchi watahoji na tukikutana nao pembeni tukiwauliza wanatoa majibu machafu.”
Alisema yeye alikuwa na shamba la ekari 10 ambazo
alikuwa anazitumia kwa kilimo na makazi, lakini ameshtuka mtu anaweka
mipaka na alipouliza viongozi walimweleza amenunua eneo hilo na ana hati
miliki.
Naye Nuhenga alisema kwa tathmini waliyofanya
vitongoji vya kijiji hicho, wamebaini takriban asilimia 80 ya ardhi ya
kijiji tayari imeuzwa na viongozi kwa wageni hususan wafugaji.
Pia, alisema licha ya wananchi kudhulumiwa ardhi
yao kwa kunyang’anywa na viongozi wa Serikali, wamekuwa hawasikilizwi
wanapopeleka malalamiko yao.
Alisema wafugaji wamekuwa wakilisha mazao ya wakulima, lakini viongozi wa vijiji hawawasilikizi.
Hata hivyo, Mtendaji wa Kijiji cha Mpanga, George
Kyelula alikana kuwapo kwa tuhuma hizo na kwamba, yeye ni mgeni ana
miezi miwili tangu ahamishiwe hapo.
Alisema hajasikia kitu kuhusu tuhuma hizo na kwamba, hayo ni majungu.
kama hicho wakati mtendaji kata ya Utengule Alex
Chawala hakutaka kuonyesha ushirikiano na wanahabari akihoji kwanini
wanachi waseme mambo hayo kwenye vyombo vya habari kabla hayajatolewa
kibali cha kuzungumza kwenye vyombo vya habari na kudai kuwa hakuna
matatizo kama hayo kwenye vijiji vyao licha ya kuwa wananchi
wamelalamika
Chanzo:Mwananchi
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment