
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa watendaji wa Tanroads.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anafuatilia kazi katika moja ya mitambo ya barabara.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ukaguzi
wa eneo lililobomolowa na mafuriko ya mvua katika daraja la Mkundi,
Dumila mkoani Morogoro.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa madereva wa Lori zinazofanya kazi katika eneo hilo.

Mtambo ukiwa kazini

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimuelekeza dereva wa lori kumwaga mawe sehemu husika.

Muonekano wa Daraja hilo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo ametembelea eneo la
Dumila ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko
ambayo yameharibu sehemu ya barabara kwenye daraja la Mto Mkundi mkoani
Morogoro.
Akiwa katika eneo hilo Waziri Magufuli baada ya kujionea hali halisi
amemwagiza Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mhandisi Crispianus Ako
pamoja na Watendaji wengine waandamizi kutoka Tanroads na Wizara ya
Ujenzi kuwepo hapo muda wote wakati kazi za kurejesha mawasiliano
zikiendelea ili kuhakikisha kuwa matengenezo hayo yanakamilika kesho
siku ya Ijumaa tayari kwa magari kuanza kupita.
Katika hatua nyingine Mhe. Magufuli ametahadharisha kuwa magari
yanayoruhusiwa kuzungukia barabara mbadala inayoanzia Dumila kupita
Kilosa hadi Morogoro ni mabasi ya abiria na magari mengine yasiyozidi
uzito wa tani 10. “Barabara hii mbadala ya kupitia Kilosa, Melela hadi
Morogoro ni ya mkoa na iko katika kiwango cha changarawe ikiwa na
madaraja yenye uwezo wa kubeba chini ya tani 10 tu, hivyo magari mengine
yote yenye uzito zaidi ya hapo yatabidi kusubiri wakati tukiendelea na
jitihada za kuifungua barabara hii mapema iwezekanavyo” amefafanua Mhe.
Magufuli.
Daraja la Mkundi liko kiasi cha kilometa 65 kutokea Morogoro mjini
kuelekea Dodoma na mikoa mingine ya kati hadi magharibi mwa nchi yetu
ikiungana na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya watu
wa Kongo.
Credit Sufiani Mafoto
0 comments:
Post a Comment