Rais Jakaya Kikwete
Aidha, Rais Kikwete amewakikishia wathirika hao kuwa serikali itahakikisha inawapatia huduma zote muhimu ikiwamo chakula na magodolo katika makazi yao ya muda.
Rais Kikwete alitoa ahadi hiyo jana baada ya kutembelea vijiji hivyo na kuzungumza na wananchi hao.
Alisema hatua ya kwanza ya ni kuhakikisha wananchi hao wanajengewa makazi ya muda ili kuendeleza maisha na kumuagiza Mkuu wa Majeshi, Janerali Davis Mwamunyange, kutuma kikosi cha jeshi hilo kusaidia kutoa huduma ikiwemo ujenzi wa makazi kwa waathirika hao.
“Mimi kama Amiri Jeshi Mkuu nimeliagiza Jeshi lije hapa na vifaa vyote kusaidia ujenzi wa makazi ya muda ili maisha yaendelee kwa wananchi wote waliokumbwa na mafuriko,” alisema Rais Kikwete.
Alisema kuwa wakati makazi hayo yakijengwa, serikali itawapa chakula na huduma mbalimbali ikiwamo ya kupatiwa maji safi na kupatiwa magodoro ya kulalalia katika makazi hayo ya muda.
“ Nimeshamugiza Waziri Lukuvi (William) kwenda katika viwanda vyote vya magodoro kuchukua ili mletewe, kama kulipa tutakuja kulipa hapo baadaye, lakini msilale chini,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumzia kuhusu huduma ya chakula, Rais Kikwete aliagiza Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, kufungua maghala ya hifadhi ya chakula ili kuwapatia wathirika hao.
“Tuna chakula cha kutosha katika maghala yetu, serikali itawapeni chakula hicho wote mliokumbwa na mafuriko hayo,” alisema Rais Kikwete.
Aidha, Rais KIkwete aliwakikishia waathirika hao kuwa serikali itaendelea kuwapatia misaada huku akiwataka wahisani mbalimbali kujitokeza kuwasaidia.
Awali akitoa taarifa kwa Rais Kikwete kuhusu mafuriko hayo,Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, alisema mpaka sasa watu 12,000 hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuharibiwa na maji.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment