Wizara ya Maliasili na Utalii kwa masikitiko makubwa inatangaza kifo cha askari mwandamizi wa wanyamapori Bw. Hassan Nindi (59) kilichotokea katika kituo cha Mtemera kilichopo katika Pori la Akiba la Selous.
Bw. Nindi alikumbwa na mauti Januari 14 mwaka huu akiwa kazini baada ya bunduki aina ya shotgun aliyokuwanayo kufyatuka na kumpiga risasi iliyosababisha mauti yake.
Bw. Nindu ameitumikia Wizara tangu mwaka 1978 katika Pori la Akiba la Selous amezikwa leo katika kijiji cha Kisaki Mkoani Morogoro.
Wizara inasikitika kuondokewa na askari huyu mchapakazi na mweledi katika kipindi hiki ambacho Wizara iko katika mapambano makali dhidi ya ujangili.
Marehemu amaeacha mke na watoto saba
Imetolewa na:
Msemaji wa Wizara,
Chikambi C. Rumisha
Wizara ya Maliasili na Utalii,
DAR ES SALAAM.
15/01/2014
0 comments:
Post a Comment