WANAKIJIJI wa kijiji cha Mandela-Magole, wilayani Kilosa,
wameziomba asasi za kiraia mkoani Morogoro kumshawishi Rais Jakaya
Kikwete kutengua maamuzi ya baraza la madiwani kuwapa wafugaji mashamba
sita yenye ukubwa wa ekari 2,509 ili kuwanusuru na mapigano.
Wakiungwa mkono na mwenyekiti wa kijiji hicho, Kilimo Njagila,
wananchi hao waliulaumu uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kwa
kuidhinisha kinyemela mashamba hayo yaliyokuwa ya Mkonge baadaye Chubuku
kwa wafugaji na kampuni ya ununuzi wa Tumbaku Dimon wakati kunahitaji
kubwa la ardhi kutokana na ongezeko la watu.
“Mchakato wa kuidai ardhi hii ulishaanza tangu mwaka 2000 hadi 2012
tukawa tumefanikiwa Rais kuyafutia umiliki, kilichotukwamisha kugawana
ni barua ya kuturuhusu kuendelea na shuguli zetu…tumefuatilia hadi
wizara ya ardhi majibu ni kuwa tusubiri itakuja na sasa ni mwezi wa 12
hatujapata jibu,” alifafanua Mwenyekiti Njagila katika mafunzo ya sheria
za ardhi yaliyoandaliwa na taasisi ya elimu na asasi ya maendeleo ya
elimu na maarifa ya ‘Greenbelt schools Trust Fund (GSTF) ya mjini
Morogoro.
Akinukuu baadhi ya barua za mchakato huo ikiwemo ya Mkurugenzi wilaya
kwa Kamishina wa Ardhi ya Juni 31, mwaka 2012 kumbu KDC/L.10/4/VOL.III/4
na barua ya Septemba 18, mwaka 2012 kumbu KDC/L.10/4/22 majibu yake ya
Agosti 28 kumbu LD/30305/102 na Desemba 3, mwaka 2012 kumbu KL/MAG/145
alisema halmashauri kupitia baraza la madiwani liliingilia mamlaka ya
kijiji hicho na kugawa mashamba hayo kinyume na sheria 1999 na 2005.
“Kama inavyoonyesha barua hii ya Mkurugenzi ya Oktoba 31, mwaka 2012
kwenda kwa Kamishna wa Ardhi kumbu KL/MAG/141 limetajwa shamba namba 35
(ekari 519), 36 (ekari 505), 37(ekari 503), 38(ekari 476), 40(ekari 256)
na 40A (ekari 250)…eneo hili linaweza kutosheleza mahitaji ya
wananchi,”alifafanua Mwenyekiti huyo.
Akijibu madai hayo, Katbu wa GSTF, John Mengele aliwataka wanachi na
viongozi kutumia elimu wanayoipata kutatua changamoto zinazowakabili
hususani katika maeneo yenye migogoro ya ardhi.
“Hatukuja kuwachonganisha kati yenu na jamii mnazoishi isipokuwa
tunawapa mwanga wa kutumia katika utatuzi wa changamoto zinazowazunguka,
kumbukeni elimu kama hii ni ghali kuipata hivyo ni vema mkaitumia kwa
usahihi katika kuzikabili changamoto,” alifafanua Mengele
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment