Morogoro
Katika Wilaya za Ulanga na Kilombero mkoani
Morogoro, baadhi ya wananchi wameeleza kufurahishwa kwao na uamuzi wa
Serikali wa kuwawajibisha mawaziri hao wakisema operesheni hiyo
ilisababisha vifo vya watu na wanyama na kwamba hata walipolalamika
hawakusikilizwa.
Mmoja wa watu aliyedai kwamba ndugu zake waliuawa
katika operesheni hiyo, Hamis Kewala alisema suala la kumalizika kwa
ujangili linahitaji umakini kwani wahusika walio wengi wamekuwa
wakitumia mbinu mpya kuua tembo na kusafirisha meno hayo, huku
wasiohusika wakiumizwa bila hatia.
Mkazi mwingine, Mohamed Nguku alisema: “Vita hii
sasa itakosa nguvu, suala la msingi ni kuhakikisha usimamizi wa hali ya
juu na umakini, halafu taratibu na sheria za nchi kwa wanaopewa dhamana
kufanya kazi hizi lazima zifuatwe na siyo kufanya wanavyojua wao”.
Agosti 12 mwaka huu, Mkazi wa Tarafa ya Mwaya
wilayani Ulanga, January Gunena alikamatwa na kupelekwa katika kambi ya
mateso iliyokuwa katika Hifadhi ya Selous na kuteswa na baadaye
alifariki dunia.
Wengine waliopatwa na mateso hayo ni madereva
wanaoendesha magari yanayofanya safari kati ya Ifakara, Mahenge na Mwaya
ambao wakiwa safarini walikuwa wakisimamishwa na askari kuhojiwa lakini
wengine wakiishia kupata vipigo na kuporwa fedha.
Chanzo;mwananchi
Chanzo;mwananchi
0 comments:
Post a Comment