Home »
» Majeruhi Mvomero wakimbizwa Muhimbili
Majeruhi Mvomero wakimbizwa Muhimbili
|
|
MAJERUHI watatu waliojeruhiwa katika mapambano ya wakulima na
wafugaji wilayani Mvomero wamekimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya
Muhimbili, jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mbali na wagonjwa hao kuhamishiwa Muhimbili katika vitengo mbalimbali
kikiwamo cha Mifupa cha Moi, pia watu wengine 14 wameruhusiwa kurejea
makwao baada ya hali zao kuendelea vizuri.
Akizungumza na Gazeti hili, Dk. Mashaka Issa, alisema waliohamishiwa
katika Hospitali ya Rufaa ni Francis William, Juma Abdi na mwingine
ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
Awali wakizungumzia hali ya machafuko hayo kwa sasa, Diwani wa kata
hiyo, Hembeti Juma Malaja na Ofisa Mtendaji wake, Charles Chikuni
alisema imetulia ingawa wananchi bado wana hofu.
Wakati huo huo, Mkuu wa Oparesheni katika Jeshi la Polisi nchini,
Paul Chagonja, alisema watu 30 wanashikiliwa na Polisi kuhusiana na
mapigano hayo.
Alisema mapigano hayo yalitokana na kukamatwa kwa ng'ombe 300 wa
Semwako Matunda wa Mpapa-Hembeti, waliokuwa wamekula mazao ya watu
wanne kijijini hapo.
Chanzo;Tanzania Daima
|
|
0 comments:
Post a Comment