Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Melela Bw
Fadhiri Mwinyimvua aliyeshjika karatasi akisoma hatua ambayo uongzi wa
kijiji hicho unakusudia kuzichukua zidi ya Dr Fulugesi aliyedaiwa
kuondoka na vifaa vya Zahanati hiyo usiku wa mamane na kutafisiliwa
kama wizi,wengini ni vigongo wa serikali na Chama cha mapinduzi wa
kijiji hicho
Umati wa wananchi wa kijiji hicho
uliokusanyika kwenye ghara cha kuhifadhia chakula baada ya kuchukizwa na
hatua ya Daktari huiyo kuondoka na vifaa vya Zahanati yao usiku mnene
Mmoja wa wananchi wa kijiji hicho
akihoji sababu za wagonjwa kutoza shilingi mia 2 kama gharama za
uchagiiaji wa mshahara wa mlini wa Zahanati hiyo
Zahanati ya kijiji cha Melele
NA DUSTAN SHEKIDELE,MVOMERO.
WANANACHI wa kijiji cha Melela kilichopo
wilaya ya Mvomero mkoani hapa,wamepinga hatua ya viongozi wao kuwatoza
ushuru wa shilingia 200 wagonjwa wanofika kwenye Zahanati ya kijiji
hicho kama gharama za kuchangia mshahara wa mlini za Zanahati hiyo.
Wakizungumza kwa jazba kwenye mkutano
uliofanyika juzi kati kwenye ghara la kuhifadhia chakula la kijiji hicho
wananchi hao kutibiwa wakidai hatua hiyo kabla ya kutibiwa wamedai
jambo hilo ni la uonezi linalowazidishia ukali wa maisha.
" Waheshimiwa tatizo lingine ni hatu ya
wagonjwa kutozwa shilingi 200 kwenye Zahanati yetu kabla ya kutibiwa
wananchi kulazimishwa kuchangia mshahara wa Mlinzi tumeliona hapa kwenye
Zahanati yetu,naamini pesa zinazopatikana kwa mwezi ni nyingi sana
ingawa siungi mkono wananchi kuradhimishwa kumlipa mlini lakini pia
ziada ya fedha hizo zina kwenda wapi na kwa nini sisi wananchi tumlipe
mshahara mlini wakati pale hopsital pia tunalipia gharama za
matibabu?"alisema mmoja wanakijiji hao
Hivi karibuni wananchi wa kijiji hicho
kilichopo wilaya ya Mvomero mkoani hapa waliitisha mkutano kinguvu na
kumshutumu daktari mkuu wa Zanahati ya kijiji hicho Dr Fulugesi kuondoka
na vifaa vya mamilioni ya shilingi vyakati za usiku.
Mwanakijiji mmoja aliyefahamika kwa jina
la Beatus Kanuti ambaye alimsindikiza mgonjwa wake kwenye Zahanati hiyo
majira ya saa 5 usiku alishuhudia mtunza stoo wa Zahanati hiyo Bw
Mlelwa akitoa vifaa 41 vya upasuaji na kumkabidhi daktari huyo muda huo
wa usiku mnene.
Jambo hilo aliluchukulia kama wizi na
kuamu kutoa taarifa kwa Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw Fadhiri
Mwinyimvua ambaye naye alitoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama wa
kijiji hicho,ambao kwa pamoja walifika kwenye Zahanati hiyo usiku huo
huo na kumkuta daktari huyo ameshatoweka.
Hivyo baada ya kushauriana walimu kwenda
nyumbni kwa daktari huyo na baada ya kupekua nyumba yake walifanikiwa
kuvikuta vifaa hivyo.ambapo ambapo usiku huo huo wananachi wa kijiji
hicho walipeana taarifa na kuamu kuitisha mkutano kujadili jambo
hilo.ambapo pia waliamualika Paparazi wa habari hizi kwenye mkutano huo
0 comments:
Post a Comment