KIONGOZI wa msikiti wa Masjid Maftah ulioko
Misufini katika manispaa ya Morogoro, Alhaj Abdul Wazir, maarufu kama Sheikh
Koba, anashikiliwa kwa mahojiano mkoani hapa kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye
umri wa miaka nane, mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi
Sabasaba.
Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda
wa Polisi mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, zilisema mtuhumiwa huyo,
anadaiwa kutenda tukio hilo chumbani kwake, Septemba tatu, majira ya saa mbili
usiku, huko Mbuyuni katika manispaa ya Morogoro.
Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumzia mazingira ya
tukio hilo, walidai kuwa Alhaj Koba, amekuwa akiishi nyumba tofauti na mkewe na
kwamba siku ya tukio mke wake alimtuma mtoto wa nduguye kupeleka chakula kwa
mumewe, lakini alichelewa kurudi, hivyo kuamua kumfuatilia kujua kulikoni.
“Alipofika kwenye nyumba anayoishi mumewe, aligonga
na kumuulizia binti huyo, lakini alielezwa kuwa alishaondoka eneo hilo, lakini
mtoto alijitokeza na kudai alikuwa bado ndani ya nyumba hiyo, na alipohojiwa
kuhusiana na uchelewaji wake, alikiri alikuwa amebakwa hivyo tukio hilo
kuripotiwa polisi,” kilieleza chanzo chetu cha habari.
Polisi walithibitisha kupokea taarifa za tukio
hilo, na kwamba uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kumfikisha mtuhumiwa
mahakamani.
Katika tukio jingine, kijana Typhory Singa,
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka
tisa, mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Lipangalala na mkazi
wa Liami Ifakara wilayani Kilombero.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Septemba nane mwaka
huu, majira ya saa nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, uchunguzi wa tukio hilo
unaendelea ili mtuhumiwa aweze kuchukuliwa hatua.
Chanzo: Tanzania
Daima
0 comments:
Post a Comment