na Lucy Ngowi, Morogoro
SERIKALI imesema mabadiliko ya tabia nchi ni tatizo la kidunia, hivyo kila mmoja anapaswa kushiriki kutoa mchango kupambana na tatizo hili.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Tathmini ya Rasilimali za Misitu, Dk. Nurdin Chamuya.
Alisema lengo la warsha inayoendelea mkoani hapa ni kuongeza uelewa wa wadau kuhusu mpango wa kupunguza uzalishaji ya hewa ya ukaa kutokana na ukataji miti ovyo na uharibifu wa misitu.
“Tutaangalia utekelezaji wa sera, mipango na mikakati ya kilimo inavyoweza kuchangia uharibifu wa mazingira ikiwemo misitu na kuongeza athari za mabadiliko ya tabia nchi,” alisema.
Alisema ili kuongeza uwezo wa kuhimili na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, upatikanaji na usambazaji wa taarifa sahihi ni jambo la msingi.
Dk. Chamuya alisema ni jambo la msingi ili jamii iweze kuchukua hatua za kuhimili na kukabiliana na mabadiliko hayo.
Katika semina hiyo washiriki wataongeza uelewa kuhusu mpango wa kupungua uzalishaji wa hewa ya ukaa kutokana na Ukataji Miti Ovyo na Uharibifu wa Misitu (Mkuhumi).
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment