Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bibi Sophia Kaduma
ameiagiza Bodi ya Sukari Tanzania, kushughulikia mara moja madai ya wakulima
wadogo wa miwa (outgrowers) katika
Kiwanda cha Sukari cha Kilombero kilichopo Mkoani Morogoro yaliotokana na miwa yao kutonunuliwa na
kiwanda.
Katika
agizo hilo, Katibu Mkuu Bibi Sophia Kaduma ameiagiza
Bodi ya Sukari Tanzania kukuta na Uongozi
wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na ule wa wakulima wadogo wa miwa ili kupata ufumbuzi wa kudumu kuhusu soko la miwa
wanayozalisha.
Aidha,
Katibu Mkuu ametoa muda wa siku saba kwa Bodi ya Sukari Tanzania iwe
imetekeleza na kutoa taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo.
Agizo
hilo limekuja kufuatia Serikali kupata taarifa kuwa Uongozi wa Kiwanda hicho umeshindwa
kununua miwa ya wakulima hao licha ya makubaliano yao ya awali ya kuzalisha
miwa na kukiuzia kiwanda kwa ajili ya kuzalisha sukari. Wakulima wamedai kuwa miwa hiyo, inakadiriwa
kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16.
Bodi
ya Sukari Tanzania imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Sukari Na. 26 ya mwaka
2001 kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 na Sheria ya Marekebisho ya Sheria za
Mazao Na. 20 ya mwaka 2009 (Crop Laws
(Miscellenous Amendments) Act).
Bodi
ya Sukari Tanzania inajukumu pamoja na mambo mengine, kusimamia na
kuratibu kilimo cha miwa na biashara ya sukari nchini, kusajili wakulima, wazalishaji wa sukari na
wafanyabiashara wa sukari.
Aidha,
Bodi ya Sukari ina dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani wa haki kwenye
soko la miwa na biashara ya sukari nchini.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara
ya Kilimo Chakula na Ushirika
Kilimo
Complex,
1
Mtaa wa Kilimo 15471
DAR ES SALAAM.
0 comments:
Post a Comment